Monday, July 2, 2012

TORRES ATWAA KIATU CHA DHAHABU, AWAPIKU GOMEZ, RONALDO

 

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Fernando Torres, ametwaa kiatu cha dhahabu kutokana na goli lake la tatu na pasi moja ya goli katika mechi ya fainali waliyoshinda 4-0 dhidi ya Italia baada ya kuingia akitokea benchi.

Torres, sawa na Mario Gomez wa Ujerumani, wamefunga magoli matatu na kutoa pasi moja ya goli lakini amepewa yeye tuzo ya mfungaji bora kutokana na kucheza muda mfupi zaidi ya wenzake.

Wachezaji wengine waliofunga magoli matatu katika fainali za Euro 2012 ni Cristiano Ronaldo (Ureno), Mario Balotelli (Italia), Mario Mandzukic (Croatia) na Alan Dzagoev (Russia), lakini magoli yao hayajawapa mafanikio wanayotaka.


VINARA WA MABAO EURO 2012
MCHEZAJI TIMU
MAGOLI DAKIKA
Fernando Torres Hispania
3 189
Mario Gomez Ujerumani
3 282
Alan Dzagoev Russia
3 253
Mario Mandzukic Croatia
3 270
Mario Balotelli Italia
3 421
Cristiano Ronaldo Ureno
3 480

No comments:

Post a Comment