Roma Mkatoliki akipagawisha baada ya fainali ya Copa Coca Cola kwenye Uwanja wa Karume leo. |
Na Sanula Athanas
NYOTA wa muziki wa hip hop,
Roma Mkatoliki leo jioni amewapagawisha kwa ‘michano’ ya hatari watu waliokuwa wamefurika
kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya fainali ya
michano ya Copa Coca Cola kati ya Mwanza na Morogoro.
Roma, Mshindi wa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa
Hip Hop 2011, alianza kuonesha makali yake muda mfupi baada ya
kumalizika kwa mechi hiyo ambayo Morogoro walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa
michuano hiyo.
Katika onesho hilo, Roma alikuwa
ameambatana na wakali wengine akiwamo Darasa aliyeshirikiana naye katika
kulipamba jukwaa.
Msanii huyo kutoka mkoani Tanga
alikuwa ‘akichana mistari’ na kucheza huku akigawa zawadi za fulana kwa
mashabiki wake na watu mbalimbali waliokuwa wamefurika kushuhudia onesho hilo.
No comments:
Post a Comment