Monday, July 16, 2012

MWIGULU: WABUNGE CHADEMA WANATISHIA KUNIUA

Mhe. Mwigulu (kulia) akiteta jambo na Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mhe. Lameck Mwigulu Mchemba, amesema kuwa kuna baadhi ya wabunge wa Chadema wamekuwa wakimpa vitisho vya kumuua kupitia simu yake ya mkononi na hivyo akataka suala hilo lijadiliwe Bungeni kwa hoja ya dharura kwani linahatarisha amani.

Mwigulu alitoa hoja hiyo asubuhi ya leo wakati wa kujadili hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Alisema kuwa wabunge hao wa Chadema wamekuwa wakimtishia kumuua kupitia ujumbe mfupi wa simu yake ya mkononi na kwamba pia anawajua wote waliomtumia meseji hizo za vitisho.

Hata hivyo, ombi la Mwigulu la kutaka suala hilo lijadiliwe bungeni kwa dharura ilipingwa na Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda, aliyesema kuwa hakuna haja ya kufanya hivyo kwani tayari polisi wameshaanza kushughulikia suala hilo linalohusishwa na tukio la kuuawa kwa kiongozi mmoja wa vijana wa CCM na watu wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia vurugu zilizoibuka  kwenye mkutano wa Chadema uliofanyika hivi karibuni katika jimbo la Mwigulu.
 

No comments:

Post a Comment