![]() |
Mhe. Spika, Anna Makinda |
![]() |
Mhe. Hamad Rashid Mohamed |
Akizungumza bungeni muda mfupi uliopita, Spika Makinda
alisema kuwa kanuni ya kutaka kuahirisha shughuli za Bunge kwa sababu ya
dharura imekuwa ikitumiwa vibaya na hivyo akaikataa hoja ya Mhe. Hamad na
badala yake akataka wabunge waendelee kujadili hoja iliyo mbele yao wakati
serikali ikisaka taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo na kuchukua hatua
zinazostahili.
Alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hoja ya dharura
huwa na mashiko pale ambapo wabunge hulazimika kwenda kuungana na wananchi
wengine kushughulikia tatizo lililotokea, akitoa mfano kuwa, ikiwa moto utatokea
eneo jirani na bunge kama Chamwino, bunge linaweza kuahirishwa kwa dharura ili
wabunge wakashirikiane na wananchi kushughulikia tatizo hilo kama vile kuzima moto
huo, na pia hata kuchangia damu pindi ikilazimika kufanya hivyo.
Baada ya Spika kutoa ufafanuzi huo, wabunge wote wa Chama cha Wananchi (CUF) na vyama vingine vya upinzani walitoka nje ya ukumbi wa Bunge kutokana na kile kilichoonekana kuwa ni kumpinga Spika Anna Makinda kwa uamuzi wake wa kupinga hoja ya Mhe. Hamad.
WAZIRI NCHIMBI AONDOA HOJA, SPIKA ANYWEA
![]() |
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Dk.Emmanuel Nchimbi. |
Hata hivyo, baada ya naibu waziri kumaliza, Waziri wa Mambo
ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi alisimama na kusoma kanuni inayompa fursa ya
kuomba kuondoa hoja yake na baada ya hapo, akamuomba Spika akubali kuahirisha
kikao cha jioni hii (kama alivyoomba Hamad) ili wakapate nafasi ya
kushughulikia ajali ya kuzama kwa boti hiyo.
Kufuatia ombi la waziri, safari hii Spika hakukataa. Alikubali kuwahoji wabunge waliobaki wa CCM juu ya hoja ya kuahirisha kikao cha jioni, na
wote walikubali.
Boti hiyo iitwayo Skagit imezama leo wakati ikiwa katika eneo la Chumbe ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar baada ya kupigwa na wimbi kali na kupinduka.
No comments:
Post a Comment