Wananchi wakiendelea na zoezi la utambuzi wa ndugu na jamaa zao leo kwenye viwanja vya Maisara, Zanzibar. |
Baadhi ya maiti za watoto waliokufa katika ajali ya boti ya Skagit |
Maiti zikishushwa garini leo baada ya kupatikana baharini katika tukio la jana la kuzama kwa boti ya Skagit. |
Habari kutoka katika eneo la uokoaji katika boti ya Skagit iliyozama
jana kwenye eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar zinaeleza kuwa hadi sasa, jumla ya
miili ya watu walioopolewa imefikia 52.
Idadi hiyo ni kati ya watu 290 waliokuwamo ndani ya boti hiyo
wakati ikisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, ambapo watu 146
kati yao wamesalimika baada ya kupatikana wakiwa hai.
Taarifa zilizotolewa bungeni leo asubuhi na Waziri wa Nchi
katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, zilieleza
kwamba kutakuwa na siku tatu za maombolezo na katika kipindi hicho, bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
BOTI SASA YAZAMA CHINI KABISA KINA CHA MITA 60
Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa zoezi la kufikia boti
hiyo ili kuangalia uwezekano wa kuopoa baadhi ya maiti zilizonasia ndani ya chombo
hico limeshindikana.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa hivi sasa, boti hiyo imekwenda
chini kabisa kwa kina cha umbali wa takriban mita 60 (zaidi ya urefu wa nusu
uwanja wa soka), hivyo kushindikana kuifikia kwani uwezo uliopo kwa binadamu ni
kwenda chini kwa umbali usiozidi mita 30.
Boti hiyo ya Skagit ambayo inamilikiwa na kampuni ya Seagul, ilizama
jana baada ya kukumbwa na dhoruba kali, ikapinduka majira ya saa 7:00 mchana
kabla ya kuzama yote baharini.
No comments:
Post a Comment