Wednesday, July 11, 2012

CHISORA AMUAHIDI HAYE NGUMI ZA "UKICHAA"

David Haye (kushoto ) na Dereck Chisora wakati wakitangaza pambano lao la Jumamosi.

Cheki mwili wewe... David Haye akionyesha jinsi mazoezi yalivyomkubali

Dereck Chisora 'akitokelezea' kibalozi.

Siku Chisora (kulia) alipomchapa kofi la uso Vitali Klitschko wakati wakipima uzito kujiandaa na pambano lao ambalo hata hivyo Chisora alidundwa.


Muunganiko wa picha zikionyesha matukio ya siku Haye na Chisora "walipoingiana miilini" wakati wa mkutano na waandishi wa habari na kusababisha kufungiwa kwao.

LONDON, Uingereza
BONDIA Dereck Chisora amemuahidi David Haye pambano la "ukichaa" wakati watakapokutana kwenye Uwanja wa Upton Park wikiendi hii.

Wawili hao waligombana kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Munich Februari, baada ya Chisora kupoteza pambano lake dhidi ya bingwa wa WBC, Vitali Klitschko, na sasa watapambana katika ulingo utakaowekwa kwenye uwanja wa soka wa West Ham Jumamosi.

"Nitakuwa kichaa kuliko wakati wowote niliopanda ulingoni," Chisora alisema.

Lakini Haye alisema: "Dereck atakumbana na KO mapema mno. Kadri akatavyokuja na vurugu ndivyo atakavyopigwa KO mapema."

Haye na Chisora waliingia miilini wakati wa mkutano wa baada ya pambano Februari, ambapo Chisora alimchapa kofi Klitschko wakati wa kupima uzito kuelekea pambano lao la kuwania mkanda wa dunia wa WBC na kisha akamtemea maji usoni kaka wa mpinzani wake, Wladimir, muda mfupi kabla ya pambano.



Miongoni mwa mabondia hao hakuna mwenye leseni ya ngumi ya Uingereza kutokana na ugomvi huo, na pambano lao limeidhinishwa na Shirikisho la Ndondi la Luxembourg.

Chisora alitabiri wiki hii kwamba atamuangusha Haye katika raundi ya saba, lakini bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Haye anaamini kwamba yuko vizuri sana hivi sasa.

"Mazoezi yangu yamekwenda poa. Nina afya tele, fiti na kasi," Haye alisema.

"Kambi hii ya mazoezi imekuwa moja ya ambazo nimeweza kufanya kila nilichopanga kwa sababu hakuna kilichokwama.

"Ni hali ambayo sijawahi kuwa hapo kabla na ninaiona tofauti. Mwalimu wangu wa kurusha ngumi amebaini tofauti pia. bahati mbaya kwa Dereck ni kwamba anapigana na Hayemaker aliye fiti kuliko wakati wowote."
 

Kocha wa Haye, Adam Booth anaamini kwamba hali aliyonayo bondia wake ya kutompenda Chisora imesaidia ratiba yake ya mazoezi.

"Hili ni binafsi," Booth alisema. "Haye anamchukia Dereck Chisora. Nimeitumia chuki dhidi ya Dereck kama kichocheo cha kumfanya ajifue zaidi. Anataka zaidi.

"Yuko katika hali inayotisha na huo ni ushahidi wa mazoezi aliyofanya."

No comments:

Post a Comment