MISRI YAOMBA KUIKABILI NGORONGORO HEROES
Chama
cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimeomba mechi mbili za kirafiki kwa
timu yao ya vijana na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya
Tanzania (Ngorongoro Heroes).
EFA
imeomba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti
maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro
Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia
mazoezi.
Ikiwa
mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) litaigharamia timu ya Misri kwa malazi, chakula, usafiri
wa ndani na sehemu ya mazoezi. Hivyo kila timu itajigharamia kwa usafiri
wa ndege na posho kwa timu yake.
Sekretarieti ya TFF inafanya uchambuzi wa gharama ili kujua ipi ni nafuu kabla ya kufanya uamuzi wa wapi mechi hizo zichezwe.
Ngorongoro
Heroes imeingia raundi ya pili ya michuano ya Afrika ambayo fainali
zake zitafanyika mwakani nchini Algeria baada ya kuitoa Sudan katika
raundi ya kwanza.
Itacheza
mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 28 mwaka huu jijini Dar es
Salaam wakati ya marudiano itakuwa Agosti 11 mwaka huu nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment