Thursday, November 28, 2013
WAKONGWE KIBAO WAPANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA GURUMO DESEMBA 14
MKONGWE wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.
Mapili amesema si yeye tu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.
Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.
Baadhi ya wakongwe wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.
Gurumo anaagwa kufuatia kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.
Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.
Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.
Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Mbizo amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25, 2013).
Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.
“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.
Sunday, November 24, 2013
KILIMANJARO STARS KUAGWA ASUBUHI
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kinaagwa kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.
Hafla ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Monday, October 28, 2013
MALINZI AMRITHI TENGA URAIS TFF....ATOA MSAMAHA
![]() |
| Oyeee! Jamal Malinzi rais mpya wa TFF |
JAMAL Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwAmo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.
Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
Wednesday, October 16, 2013
KUZIONA SIMBA, YANGA SH.5,000
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
Sunday, October 6, 2013
UZINDUZI WIKI YA MITINDO VODACOM ULIVYOFANA
MIMI NDO' BIBI BOMBA
KAMPENI YA “NANI MTANI JEMBE” YAZINDULIWA DAR
| Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
| Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiongea wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
| Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
| Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
BIA ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100 zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki maalum mtandaoni.
ü •
ü Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.
ü Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
ü Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
ü Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.
ü Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
ü Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo katika miradi yake ya maendeleo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi.
Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga.
Kampeni hii itafika kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.
MCHAKATO EPIQ BSS UNAVYOSONGA
| Mshiriki Merisa John ambae alichaguliwa kwa njia ya simu (Wild Card) kuingia katika shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) akiimba kwa hisia mbele ya majaji wa shindano hilo |
| Jaji Madam Ritha (katikati) akifurahia jambo pamoja na majaji wenzake Master Jay (kulia) na Salama Jabir wakati wa shindano hilo. |
| Washiriki wakisikiliza maoni kutoka kwa majaji ambapo wote waliambiwa kuwa wanaendelea kubakia katika jumba hilo |
PAMBANO LA RUVU, SIMBA LAINGIZA MIL 75/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 75,692,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh. 3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,066,841.66.
Tuesday, October 1, 2013
REDD'S MISS TANZANIA ALIPOTEMBELEA TBL
| Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kampuni ya bia nchini (TBL). |
| Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa mkurugenzi mkuu wa TBL, Robin Goestzche (kulia). |
| Mkurugenzi Mkuu wa TBL nchini Tanzania, Robin Goestzche akimpongeza Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa na kushoto ni Mkugenzi wa Masoko wa TBL Kushila Thomas. |
| Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa mkurugenzi mkuu wa TBL, Robin Goestzche (kulia). |
REDD’S Miss Tanzania, Happiness Watimanywa jana alitembelea rasmi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) walio wadhamini wa shindano hilo, ambapo alikutana na uongozi wa juu ili kujitambulisha.
Katika ziara hiyo, Happiness alifuatana na mshindi wa pili, Latifa Mohammed, mshindi wa tatu, Clara Bayo pamoja na Kamati ya Redd’s Miss Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kukutana na mrembo huyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goestache alisema, wao kama wadhamini wakuu wanajisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya Redd’s Miss Tanzania, huku akimsifu mrembo huyo kwa ushindi wake.
“Kila mmoja kati yetu anajua shindano lilivyokuwa gumu, warembo wote walikuwa na sifa na ninawapongeza ninyi mlioshinda na tunawakaribisha katika familia ya TBL,” alisema.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushillah Thomas, naye alitumia fursa hiyo kuwapongeza warembo hao na kusema ana imani kubwa nao watafanya vizuri zaidi katika kipindi chao.
Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, toka waanze kudhamini shindano hilo wamepata mafanikio makubwa mno, huku kukiwa na kazi nyingi za jamii wanazozifanya na warembo waliofanikiwa kutwaa taji hilo.
Happiness naye aliishukuru TBL kwa kudhamini shindano hilo na kusema anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya familia ya Redd’s.
“Kwa kiasi kikubwa nawashukuru kutokana na kudhamini shindano hili kwa muda wa miaka 13, kwani mmesaidia mengi kwa warembo na najivunia kuvaa sura ya Redd’s.”
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Friday, September 27, 2013
BRIGITTE ANG'ARA MISS WORLD, KUWANIA TAJI LA DUNIA LEO
![]() |
| Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lyimo |
Wakati warembo 131 leo wanawania taji la urembo wa Dunia (Miss World), Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred Lyimo ameng’ara kwa kushinda nafasi ya tatu katika kipengele cha Urembo wenye malengo maalum (Beauty With Purpose).
Mrembo huyo amewashinda warembo 129 waliwania taji hilo ambalo ni kubwa baada ya lile la Miss World. Kilichompa ushindi mrembo huyo ni mradi wake wa kujenga bweni la watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao upo Buhangija mkoani Shinyanga umemgharimu mrembo huyo zaidi ya sh milioni 60.
Katika mashindano hayo, mrembo wa Nepal, Ishani Shrestha alishika nafasi ya kwanza na ya pili ilishikwa na mrembo wa Australia, Erin Holland. Warembo wengine waliomaliza katika 10 bora ya mashindano hayo ni Noémie Happart (Ubelgiji) aliyeshika nafasi ya nne, Sancler Frantz (Brazil namba 5), Marine Lorphelin (Ufaransa) nafasi sita.
Pia katika oridha hiyo ya washindi wapo warembo wa Ghana, Uingereza, India na Aruba ambao walishika nafasi ya saba, nane, tisa na ya kumi.
Katika kipengele hicho, warembo hao walifanya kazi za jamii ambazo zina mtazamo wa kimaifa ambapo mbali ya kufanya, mrembo husika anatakiwa kutoa maelezo ya mradi huo mbele ya majaji. Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga alisema kuwa matokeo hayo ni faraja kwa mashindano ya Miss Tanzania kwani yameiweka Tanzania katika chati ya hali ya juu Duniani.
Lundenga alisema kuwa Brigitte ambaye pia ni Miss Sinza aliweza pia kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na sura nzima ya Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.
“Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufanya vyema katika mashindano ya dunia baada ya Nancy Sumari mwaka 2005 alipomaliza katika fainali ya warembo tano bora kati ya warembo 120 duniani. Nancy alishinda taji la mrembo bora wa Afrika, hivyo Brigitte ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri leo katika fainali mashindano hayo (Miss World) yanayofanyika mjini Bali, Indonesia, naomba tumuombee aibuke kidedea,” alisema Lundenga.
Tuesday, September 10, 2013
WAREMBO WAENDELEA NA ZIARA
Sunday, September 8, 2013
POULSEN: KUKOSEKANA NYOTA KUMETUMALIZA
Kocha Kim Poulsen amesema kukosekana kwa wachezaji tisa muhimu ni mojawapo ya sababu ya kushindwa mechi ya Jumamosi na akaiomba TFF kuhakikisha kuwa wachezaji wanaocheza nje wakiitwa wanakuja nyumbani kucheza.
Kocha huyo aliyasema hayo Mjini Banjul mara tu baada ya mchezo na Gambia ambapo wenyeji walishinda kwa bao 2-0 katika mechi ya mwisho ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia.
Amesema alikosa wachezaji tisa muhimu amabapo wengine hawakufika kabisa kutoka wanakocheza soka la kulipwa na wengine walikuwa majeruhi.
“Nimeambiwa Gambia waliita wachezaji kumi na moja kutoka nje kwa sababu walitambua umuhimu wa kushinda mechi hii na sisi tulikosa karibu timu nzima,” alisema na kusema ni bora TFF wahakikishe kuwa wachezaji hawa wanapohitajika hasa kwenye mechi za kufuzu kucheza Kombe la Afrika, wanapatikana kwa wakati.
“Tumeijenga hii timu tukiwa na malengo ya kufuzu kucheza fainali hizo za Kombe la Afrika kwa hivyo ni muhimu sana wawepo wanapoitwa,” alisema Poulsen.
Wachezaji wazoefu wa Stars waliokosa mechi hiyo ni, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Salum Abubakar, John Boko, Mwinyi Kazimoto, Shomari Kapombe na Aggrey Morris.
Alisema baadhi ya hawa wachezaji ambao ni vijana, wamejipatia uzoefu mkubwa pamoja na kwamba walifanya makosa kadhaa uwanjani ambayo anaamini kama wachezaji wenye uzoefu kidogo wangekuwepo wangeweza kudhibiti ile hali kwa nammna moja au nyingine.
Hata hivyo, amesema licha ya timu yake kushindwa na Gambia hajakata tama kwani malengo aliojiwekea tangu mwanzo ni kufuzu kucheza fainali za Kombe la Afrika 2015, jambo ambalo hata TFF na mdhamini, Kilimanjaro Premium Lager wanalitambua na wanaunga mkono.
Amesema inasikitisha kupoteza mechi lakini watanzania lazima waelewe kuwa malengo ni ya muda mrefu na timu inaendelea kuimarika siku hadi siku.
Alisema huu sio muda wa kulaumu na kukata tamaa kwani safari bado ndefu na tayari kuna dalili nzuri zinaonekeana hasa tangu Taifa Stars ipate udhamini mpya wa Kilimanjaro Premium Lager ambao unawezesha mambo mengi kufanyika sasa kwani imewekeza zaidi ya bilioni 15 kwa miaka mitano.
“Mechi hizi za Kombe la Dunia zimetupa uzoefu kwani Tumeweza kucheza na timu kubwa kama Ivory Coast na Morocco na kuonesha uwezo mkubwa zaidi nah ii inaonesha uwa timu imeimarika kabisa,” alisema.
Kabla ya mechi hiyo baadhi wa wananchi wa Gambia walionesha kutokuwa na imani na timu yao baada ya kutofanya vizuri katika mechi zilizopita.
Geoffrey Kaishozi ambaye ni Mtanzania anaefanya kazi Gambia alisema alifurahishwa na jinsi Stars ilicheza katika kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili mchezo ulibadilika baada ya Gambia kupata goli katika dakika ya 45 na lingine katika kipndi cha pili.
“Tumesikitika kuwakosa wachezaji wengi tuliowazoea nap engine kuwepo kwao kungeleta utofauti katika mechi hii,” alisema na kuongeza kuwa ni muhimu wachezaji wale muhimu wawepo katika mechi muhimu kama hizi.
Naye Francis Mushi alisema alienda uwanjani na matumaini kuwa Taifa stars ingeshinda hasa baada ya kuifunga Gambia 2-1 katika mechi ya awali nyumbani.
“Tulicheza vizuri katika kipindi cha kwanza lakini katika kipindi cha pili tulilemewa na tukaamka dakika za mwisho za mpira lkini hatukufanikiwa kupata goli,” alisema na kuongeza kuna umuhimu wa timu kukaa pamoja kwa muda mrefu ili wachezaji waweze kuelewana vizuri uwanjani.
Alisema Gambia pia hawakucheza katika kiwango chao cha kawaida kwa hivyo wengi walitegemea Taifa Stars ingeshinda.
Emmanuel Mtaki ambaye pia anafanya kazi Gambia alisema kulikuwa na makosa mbalimbali kama mabeki kutowadhibiti vizuri washambuliaji wa Gambia, wachezaji wa katikati kutotowa pasi za uhakika ili iwapate washambuliaji na pia nguvu ya ushambuliaji kuwa ndogo.
“Wachezaji wetu lazima wajiamini hata kama wenzao wengne wanakosa, waliopo wajiamini na wafanye kazi uwanjani,” alisema.
Magoli yote ya Gambia katika mchezo wa Jumamosi yalifungwa na nahodha wa timu hiyo Mustafa Jarjue ambaye alicheza mpira wa hali ya juu.
Stars inatarajiwa kuwasili nyumbani Jumatatu saa nane mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.
Sunday, August 25, 2013
MECHI YA YANGA, ASHANTI YAINGIZA MIL 102/-, YA SIMBA MIL.44
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Ashanti United iliyochezwa jana (Agosti 24 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 102,856,000, wakati ya Simba dhidi ya Rhino Rangers iliyoisha kwa sare ya 2-2 iliyochezwa Tabora iliingiza Sh. milioni 44.
Watazamaji 17,744 walikata tiketi kushuhudia mecchi hiyo namba moja ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa mabingwa watetezi Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 24,400,102.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,689,898.31.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 12,406,831.75, tiketi sh. 4,453,890, gharama za mechi sh. 7,444,099.05, Kamati ya Ligi sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,722,049.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,894,927.41.
Saturday, August 24, 2013
USAJILI WA WARUNDI WA SIMBA WAKWAMA, JAVU NAYE AKWAMA YANGA
![]() |
| Tambwe Amisi akibeba kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) wakati akiwa na Vital'O jijini Darfur hivi karibuni. |
KLABU ya Simba haitaweza kuwatumia nyota wake wote watano wa kigeni katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kutokana na kukosa vibali vya uhamisho wa kimataifa ITC au vibali vya kufanyia kazi nchini, wakati pia Hussein Javu hataweza kuichezea Yanga dhidi ya Ashanti leo kwa kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo, straika Amisi Tambwe na beki Gilbert John Kaze kutoka Vital'O ya Burundi hawataweza kuichezea Simba kwa vile hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini, wakati pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha kufanya kazi nchini, Joseph Owino tayari ITC yake imepatikana lakini hana kibali cha kufanya kazi nchini na ni lazima Simba kwanza imfanyie uhamisho straika Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC.
Vilevile Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim 'Messi' kutoka Coastal Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20).
Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
Wachezaji waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na ITC.
Kwa ujumla, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.
Klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja mbalimbali nchini.
JKT Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans). Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto (Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata (African Lyon).
Pia Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
Tanzania Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro.
Kagera Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto Africans).
Pia Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work permit).
Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif (African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).
Oljoro JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
Nayo Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif (Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20.
Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz Chibwabwa (Villa Squad).
Kwa mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
Pia TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru (free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.
Friday, August 23, 2013
MAJINA YA WAOMBAJI UONGOZI TFF, TPL BOARD YAWEKWA WAZI
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi.
Kipindi cha pingamizi kinaanza kesho (Agosti 24 mwaka huu) hadi saa 10 kamili jioni ya Agosti 26 mwaka huu ambapo waweka pingamizi wanaruhusiwa kupitia taarifa za wale wanaokusudia kuwawekea pingamizi kabla ya kuwasilisha pingamizi husika.
Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi, Agosti 27 hadi 29 mwaka huu ni wawekaji pingamizi na wawekewa pingamizi kufika mbele ya Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya kusikiliza pingamizi.
Waombaji kuwania uongozi katika TFF ambao majina yao yamebandikwa ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard J. Rukambura (urais). Nafasi ya Makamu wa Rais ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Walace John Karia.
Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda ni Kanda Namba Moja (Kagera na Geita) ni Abdallah Hussein Mussa na Kaliro Samson. Kanda Namba Mbili (Mara na Mwanza) ni Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Kalwizira Lufano.
Kanda Namba Tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko na Stanslaus Haroon Nyongo. Kanda Namba Nne (Arusha na Manyara) ni Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii Ali.
Kanda Namba Tano (Kigoma na Tabora) ni Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamisi Kitumbo. Kanda Namba Sita (Katavi na Rukwa) ni Ayoub Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo, Nazarius A.M. Kilungeja. Kanda Namba Saba (Iringa na Mbeya) ni Ayoub Shaibu Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Samson Lugenge, Elias Lusekelo Mwanjala, Eliud Peter Mvella na John Mwachendang’ombe Kiteve.
Waombaji wa Kanda Namba Nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Kanda Namba Tisa (Lindi na Mtwara) ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder.
Kanda Namba Kumi (Dodoma na Singida) ni Charles Komba, Hussein Zuberi Mwamba na Stewart Ernest Masima. Kanda Namba 11 (Morogoro na Pwani) ni Farid Salum Mbarak, Geoffrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala na Twahil Twaha Njoki.
Wanaowania kuteuliwa kugombea kupitia Kanda Namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed wakati Kanda Namba 13 (Dar es Salaam) ni Alex Chrispine Kamuzelya, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa upande wa TPL Board waliotangazwa kuomba kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).
Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
YANGA, SIMBA VITANI VPL JUMAMOSI
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya City iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini, Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi itasimama kupitisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul. VPL itaingia mzunguko wa tatu Septemba 14 mwaka huu.
TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUANZA MZUNGUKO WA NNE
Tiketi za elektroniki zitaanza kutumika katika mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaoanza Septemba 18 mwaka huu. Tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda hiyo imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi hizo katika viwanja vyote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, hivi sasa Serikali ambayo ndiyo inamiliki Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na CRDB zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja huo ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo.
Mfumo (system) iliyoko kwenye uwanja huo inapishana na ule utakaotumiwa na CRDB, hivyo pande husika zinashughulikia suala hilo ili mifumo hiyo iweze kuingilia.
Pia mashine za kuchapia (printer) kwa ajili ya tiketi ambazo CRDB wameziagiza kutoka nje ya nchi zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.
Hivi sasa CRDB inashughulikia ufungaji wa vifaa vya matumizi ya tiketi za elektroniki iwemo turnstiles kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao mwanzoni hakuwemo kwenye mpango huo kutokana na Mkoa wa Tabora kutokuwa na timu ya Ligi Kuu.
MISS TANZANIA BRIGITTE AANZA UJENZI BWENI LA WANAFUNZI ALBINO SHINYANGA
![]() |
| Miss Tz 2012 Brigette Alfred akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni la wavulana shule ya msingi Buhangija akiwa pamoja na afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika. |
![]() |
| Miss Tanzania Brigitte Alfred (wa pili kulia) akiwa na afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na wadau ndani ya jengo la bweni la wavulana katika shule hiyo. |
MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija katika wilaya ya Shinyanga.
Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50.
Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali.
Briggite alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Alisema kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo wenye Malengo Maalum (Beauty with Purpose) na yeye kuamua kufanya kwa vitendo.
“Ni faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.
Alisema kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jengo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.
Brigitte pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.
“Nilipata msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake.
Nyamubi alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa na ni msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.
Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachukua wakati wa likizo.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo, Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.
NEYMAR AFURAHIA GOLI LA KWANZA
![]() |
| Neymar wa Barcelona akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Atletico de Madrid wakati wa mechi yao ya kwanza ya Supa Copa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Agosti 21, 2013. |
NEYMAR ameelezea furaha yake kufunga goli lake la kwanza la kimashindano tangu ajiunge na Barcelona katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mechi yao ya kwanza ya Supa Copa.
Mbrazil huyo aliingia kutokea benchi Jumatano na kufunga goli la kusawazisha baada ya nyota wa zamani wa Barca, David Villa kuifungia timu yake mpya goli la kuongoza.
"Nina furaha kwamba nilifunga goli la kusawazisha. Ilikuwa ni mechi ngumu dhidi ya wachezaji bora,” alisema.
"Atletico ni timu kubwa, na wameonyesha tena katika mechi hii. Ni matokeomazuri na sasa tunapaswa kumaliza kazi nyumbani."
Subscribe to:
Posts (Atom)


.jpg)








