Sunday, June 16, 2013

RONALDO AMWAMBIA BALOTELLI: USIUE KIPAJI CHAKO KAMA ADRIANO

Ronaldo de Lima akiwa matembezi na rafikiye wa kike, DJ Paula Morais
Ronaldo de Lima akiwa matembezi na rafikiye wa kike, DJ Paula Morais
Ronaldo de Lima akifanya shopping na rafikiye wa kike, DJ Paula Morais, mjini Madrid, Hispania
Balotelli akiwa matembezi na rafikiye wa kike
Mario Balotelli akijifua na wenzake wa timu ya taifa ya Italia katika maandalizi ya kushiriki Kombe la Mabara kwenye Uwanja wa Estadio Joao Havelange mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Mario Balotelli akijifua na wenzake wa timu ya taifa ya Italia katika maandalizi ya kushiriki Kombe la Mabara kwenye Uwanja wa Estadio Joao Havelange mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Mario Balotelli akijifua na wenzake wa timu ya taifa ya Italia katika maandalizi ya kushiriki Kombe la Mabara kwenye Uwanja wa Estadio Joao Havelange mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Mario Balotelli akijifua na wenzake wa timu ya taifa ya Italia katika maandalizi ya kushiriki Kombe la Mabara kwenye Uwanja wa Estadio Joao Havelange mjini Rio de Janeiro, Brazil.


RONALDO de Lima amemshauri mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli, asiache kipaji chake kipotee kama nyota wa zamani wa Inter Milan na Brazil, Adriano.

Aliliambia Gazzetta dello Sport: “Balotelli amejaliwa kipaji kikubwa, anajua namna ya kuufanya mpira katika hali fulani na kuutumbukiza wavuni.

"Lakini hapaswi kuridhika na alipofikia na hapaswi kutumia umri wake kama kisingizio cha kufanya vitu vya kipuuzi uwanjani.

“Kama straika anajua kucheza, lazima wapinzani watamchokoza kwa kumchapa viatu. Nafahamu vyema hili, kama ningekuwa narudishia kila anayenipiga kiatu... sote tunafanya mambo ya kijinga maishani mwetu, lakini ni lazima tubaini kwamba ni wakati wa kuacha. Hesabu hadi tano kabla ya kujibu.

"Ananikumbusha Adriano, ingawa suala lao ni tofauti. Adriano alikuwa na ufundi na nguvu, hivyo angefanya chochote uwanjani, lakini kulikuwa na wakati uzalendo unamshinda."

"Ushauri wangu kwa Balotelli ni huu: usipoteze kipaji chako. Kwenye Uwanja wa Maracana unaweza kujua nani mchezaji wa kweli na nani anafulia, hivyo namwambia asipagawishwe na hali hiyo. Kucheza pale kunakupa mizuka, kwa sababu ni moja ya viwanja bora zaidi duniani. Sikuwahi kufunga goli la kimashindano katika uwanja wa Maracana."

NEYMAR AFUNGA LA UFUNGUZI MABARA BRAZILI IKIUA 3-0

Neymar akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Japan katika mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mabara nchini Brazil jana usiku
Kitu "kunyavu"... Kipa wa Japan,Kawashima akiruka bila ya mafanikio kujaribu kuokoa shuti la Neymar lisitinge wavuni
Golden Boy kipenzi cha walimbwende akishangilia goli lake jana usiku

NEYMAR alifunga goli la kwanza la michuano ya Kombe la Mabara usiku wa kuamkia leo wakati wenyeji Brazil walipoanza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Japan katika mechi ya ufunguzi.

Goli kali la Neymar katika dakika ya tatu liliwajengea Brazil kujiamini kabla ya Paulinho kuongeza la pili katika dakika ya tatu ya kipindi cha pili. Mtokea benchi Jo, ambaye aliwahi kuichezea Manchester City, alikamilisha ushindi katika dakika ya tatu ya majeruhi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada yamechi hiyo, Neymar (21) alielezea furaha yake kwa kiwango chake binafsi na kwamba anaona timu sasa inazidi kukomaa.

"Nina furaha nimefunga," alisema Neymar ambaye alifunga goli lake la kwanza katika mechi 10 zilizopita za klabu na taifa. "Daima huwa nasema nataka kuboresha kiwango changu, na nataka timu icheze kama kikundi."

Neymar, ambaye sasa ameifungia timu yake ya Brazil magoli 21 katika mechi 35 alizocheza, alipumzishwa kuelekea mwishoni mwa mechi baada ya kupata maumivu kidogo na mashabiki uwanja mzima wakasimama kumpigia makofi kwa heshima lakini alisisitiza kwamba hakuna cha kuhofia.

"Niko fiti na niko tayari kwa mechi ijayo, na nyingine zote," alisema. "Daima nafikiria kuhusu familia yangu na napata mizuka ya kucheza."

Mashabiki 67,000 waliohudhuria walishuhudia polisi wakilipua mabamu ya machozi kwa waandamanaji wenye hasira wakipinga gharama kubwa zilizotumika kujenga viwanja kwa ajili ya michuano hiyo na ya fainali za Kombe la Dunia mwakani badala ya kutumika kutatua matatizo ya kijamii.

Kikosi cha kocha Luiz Felipe Scolari kinafukuzia ubingwa wa tatu mfululizo wa Kombe la Mabara baada ya kuutwaa katika michuano iliyopita ya 2005 na 2009.

Brazil watatinga nusu fainali kama watashinda dhidi ya Mexico Jumatano.
----------------

MARIETA ASHINDA REDD'S MISS CHANG'OMBE


Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa (katikati) akiwa na uso wa furaha mara baada ya kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma. Kushoto ni mshindio wa pili Sabrina Juma kutoka mkoani Tabora na kulia ni mshindi wa tatu Jackline.

MREMBO Marieta Boniface juzi usiku alitwaa taji la Redd’s Miss Chang’ombe 2013 katika kinyang’anyiro kikali kilichofanyika kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Marieta aliwashinda warembo wengine 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Kutokana na ushindi huo, Marieta alizawadiwa pikipiki yenye thamani ya Sh. milioni 1.5 ambayo ilitolewa na wadhamini wenza Kampuni ya Kishen Enterprises Ltd.

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi ndiye aliyemkabidhi zawadi hiyo na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na shindano hilo na yupo tayari kulisaidia zaidi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa taji, Marieta alisema anaamini kwa dhati atafanikiwa kufika mbali zaidi kwani amedhamiria kuhakikisha anaibeba Chang’ombe katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.