Niklas Bendtner |
Park Young |
Sebastien Squillaci |
KOCHA Arsene Wenger wa Arsenal
amesema kuwa wachezaji Niklas Bendtner, Park Young na Sebastien Squillaci wako
mbioni kuondoka na kwamba pia atazungumza na winga Andrey Arshavin ili kuamua
hatma yake klabuni hapo.
Arshavin ambaye ni straika
mwenye miaka 31 alimalizia nusu ya pili ya msimu uliopita akiwa kwa mkopo
katika klabu yake ya zamani ya Zenit St Petersburg ya Urusi, ikiwa ni baada ya
kiwango chake kupondwa na mashabiki wengi wa Arsenal.
Zaidi ya hayo, nahodha huyo wa
Urusi amekuwa akitarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo katika kipindi hiki cha
majira ya kiangazi ili zipatikane fedha za kusajili nyota wengine zaidi baada
ya kuwasili kwa wachezaji wapya Lukas Podolski na Olivier Giroud.
Hata hivyo, Wenger ahajafuta
uwezekano wa kuendelea kumbakiza Arshavin, mchezaji aliyemnunua kwa paundi za
England milioni 15 (Sh. bilioni 37) wakati wa usajili wa dirisha dogo la
Januari, 2009, licha ya kwamba hakujumuishwa katika kikosi cha klabu hiyo
kilichokwenda katika ziara yao ya Mashariki ya Mbali.
"Arshavin, inategemea.
Tunapaaswa kukaa wote chini na kufanya mazungumzo. Anaweza kuendelea kuwa nasi
klabuni," alisema Wenger kuiambia Daily Mail.
Wachezaji ambao hadi sasa
wanaonekana kuwa ni mzigo katika kikosi cha Wenger ni pamoja na beki wa timu ya
taifa ya Ufaransa, Sebastien Squillaci na mshambuliaji wa Korea Kusini
Chu-Young Park, wote wakishindwa kuonyesha makali yao tangu walipotua wakitokea
katika klabu za Sevilla na Monaco, wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark,
Nicklas Bendtner, ambaye msimu uliopita aliichezea Sunderland kwa mkopo, pia
yuko mbioni kuhama.
"Bendtner,
Squillaci na Park wako njiani kuondoka na kwenda kucheza kwingine,"
aliongeza Wenger.
No comments:
Post a Comment