Rais wa CWT, Gratian Mukoba (kushoto) |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa |
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi
katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam imeshindwa kutoa uamuzi wa mgogoro uliopo baina
ya serikali na walimu na ambao ndio uliozaa mgomo wa walimu usio na kikomo kwa nchi nzima kuanzia jana.
Jaji Sophy Wambura wa Mahakama
hiyo aliahirisha shauri hilo hadi Alhamisi (Agosti 2) wakati atakapolitolea uamuzi
baada ya kupitia hoja za pande zote mbili .
Awali, wakili wa serikali
aliiomba mahakama hiyo kukiamuru Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kusitisha
mgomo huo ulioanza jana kwani ni batili.
Wakili wa CWT
alisema kuwa mgomo huo ni halali kwani umefuata sheria na taratibu zote kabla
ya kuitishwa kwake.
CWT iliitisha mgomo wa walimu kuanzia
jana baada ya mgogoro wake na serikali kushindwa kupatiwa ufumbuzi na msuluhishi.
Chama hicho kinataka serikali iongeze
mshahara wa walimu kwa asilimia 100, kuongeza posho za walimu kwa asilimia 50 na
55 kwa walimu wa sayansi na pia kuwalipa walimu posho ya mazingira magumu kwa kiasi
cha asilimia 30 ya mshahara.
No comments:
Post a Comment