Thursday, November 28, 2013
WAKONGWE KIBAO WAPANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA GURUMO DESEMBA 14
MKONGWE wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.
Mapili amesema si yeye tu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.
Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.
Baadhi ya wakongwe wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.
Gurumo anaagwa kufuatia kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.
Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.
Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.
Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Mbizo amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25, 2013).
Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.
“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.
Sunday, November 24, 2013
KILIMANJARO STARS KUAGWA ASUBUHI
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kinaagwa kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.
Hafla ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Monday, October 28, 2013
MALINZI AMRITHI TENGA URAIS TFF....ATOA MSAMAHA
Oyeee! Jamal Malinzi rais mpya wa TFF |
JAMAL Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwAmo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.
Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
Wednesday, October 16, 2013
KUZIONA SIMBA, YANGA SH.5,000
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
Sunday, October 6, 2013
UZINDUZI WIKI YA MITINDO VODACOM ULIVYOFANA
MIMI NDO' BIBI BOMBA
KAMPENI YA “NANI MTANI JEMBE” YAZINDULIWA DAR
Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiongea wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
Mashabiki Simba na Yanga wakicheza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam leo. |
BIA ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100 zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki maalum mtandaoni.
ü •
ü Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.
ü Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
ü Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
ü Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.
ü Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
ü Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo katika miradi yake ya maendeleo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi.
Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga.
Kampeni hii itafika kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)