Thursday, October 4, 2012

RONALDO, KAKA, RAMOS WACHEKELEA USHINDI WAO REAL MADRID WA 4-1 DHIDI YA AJAX… ARSENAL, PORTO, MILAN MWENDO MDUNDO … BALOTELLI AIOKOA MAN CITY ISICHEZEE KICHAPO KUTOKA KWA BORUSSIA DORTMUND


Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akimtoka Ricardo Van Rhijnwa wa Ajax wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters).

Ronaldo akipiga shuti na kufunga goli la kwanza wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters).

Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid baada ya kufunga goli la tatu wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters).

Safi mwana...! Sergio Ramos akimpongeza Ronaldo baada ya kuifungia Real goli la nne wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters).
Benzema wa Real Madrid akishangilia goli alilofunga dhidi ya Ajax jana usiku pamoja na Marcelo wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters).

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishangilia kwa kubusu mpira baada ya kupiga hat-trick  na kuipa timu yake ushindi wa 4-1 katika mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters) 


Sergio Aguero wa Manchester City akichuana na Mario Gotze wa Borussia Dortmund wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters)

Neven Subotic wa Borussia Dortmund akishika mpira unaopigwa na Sergio Aguero wa Manchester City na kusababisha penati iliyofungwa na Mario Balotelli wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, jana Oktoba 3, 2012 in Manchester, England. (Picha: Reuters)

Juu, Mario Balotelli wa Manchester City akipiga penati na kufunga. Hapa Balotelli anaonekana akimdhihaki kipa Roman Weidenfeller wa Borussia Dortmund baada ya kufunga kwa penati hiyo wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, jana Oktoba 3, 2012 in Manchester, England. (Picha: Reuters)


Gervinho wa Arsenal akimtoka Giannis Maniatis wa Olympiacos wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters)

Gooooooohh....! Gervinho wa Arsenal akipiga shuti na kufunga goli la kwanza dhidi ya Olympiakos wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters)
Weweeee....! Gervinho akishangilia goli alilofunga dhidi ya Olympiakos

Lukas Podolski wa Arsenal akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Olympiakos .
Aaron Ramsey wa Arsenal akipongezwa na Mikel Arteta baada ya kufunga goli la tatu dhidi ya Olympiakos wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters)
Porto wakishangilia goli lao la ushindi dhidi ya PSG wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mjini Porto, jana Oktoba 3, 2012.
Zlatan Ibrahimovic wa PSG akipiga kichwa kuelekea lango la Porto wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyochezwa mjini Porto, Ureno jana usiku Oktoba 3, 2012.
AMSTERDAM, Uholanzi
Cristiano Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos wameelezea furaha yao kutokana na ushindi walioupata Real Madrid ugenini wa 4-1 dhidi ya Ajax na kusema kwamba wamepania kushinda pia katika mechi ijayo ya ugenini dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Ronaldo alikuwa shujaa wa kikosi cha Jose Mourinho baada ya kufunga ‘hat-trick’ huku bao jingine likiwekwa wavuni na Karim Benzema, wakati Kaka na Sergio Ramos walipangwa katika kikosi cha kwanza licha ya kuonekana kupoteza mvuto kwa kocha wao katika siku za hivi karibuni.

"Nimefurahi sana kwa sababu tumecheza vizuri na kushinda," Ronaldo ameiambia Canal+.

"Kwangu mimi, kufunga mabao matatu ni muhimu. Tulicheza mechi vizuri sana na hilo ni muhimu kwetu katika kujipa hali ya kujiamini kabla ya mechi yetu ijayo (dhidi ya Barcelona). Ni muhimu sana kurejea nyumbani na mpira lakini ni muhimu zaidi kwa timu nzima kwa sababu bila wenzangu nisingeweza kufunga magoli haya."

Barcelona inaweza kuongeza tofauti ya pointi baina yao kufkia 11 kama itashinda dhidi ya Real MadridJumapili, lakini Ronaldo anaamini kwamba timu yake ndiyo itakayoshinda.

"Ninajiamini kwamba tutapata matokeo mazuri katika sehemu ngumu kushinda, ya Uwanja wa Camp Nou. Wana timu nzuri sana na hakutakuwa na tofauti kubwa," alieleza Ronaldo, ambaye magaoli yake matatu jana yalimfanya apate ‘hat-trick’ ya kwanza katika ligi ya klabu bingwa Ulaya na pia kuongeza akaunti yake ya mabao katika michuano hiyo kufikia 42.

Real sasa wanaongoza katika kundi lao la D baada ya kufikisha pointi sita katika mechi mbili, wakifuatiwa na Borussia Dortmund waliofikisha pointi nne baada ya kupata sare ya 1-1 katika mechi yao ya ugenini jana usiku pia dhidi ya Manchester City. Ajax wanaburuta mkia baada ya kufungwa katika mechi zote mbili.
    
Nafasi ya Kaka katika kikosi cha kwanza imekuwa ngumu msimu huu lakini kiungo huyo mchezeshaji wa Brazili  amejipanga kuhakikisha kwamba anapata namba katika kikosi cha Real Madrid.

"Kidogo ilinishangaza, lakini ni ushindi binafsi unaotokana na kujituma. Niko tayari kwa kocha, vyovyote atakavyonihitaji.

"Barcelona ni moja kati ya wapinzani wetu wa moja kwa moja, na hiyo inamaanisha kwamba mechi dhidi yao ni muhimu sana."

Wakati huohuo, baada ya ‘kuchenjiana’ hadharani na kocha wake Jose Mourinho, Sergio Ramos amesema kwamba sasa wawili hao wamemaliza tofauti baina yao na nahodha huyo msaidizi anaamini kwamba timu yake inaweza kuendelea na kasi yao ya ushindi na kiwango kizuri uwanjani.

"Bifu na Mourinho limeisha, na nimefurahia ushindi wetu katika Ligi ya Klabu Bingwa, jambo ambalo ni la muhimu zaidi kwa timu," amesema beki huyo wa kimataifa wa Hispania.

"Ulikuwa ni ushindi muhimu dhidi ya timu ngumu, lakini sasa tunapaswa kugeukia La Liga. Mechi ya Clasico inakuja na siku zote huwa ni maalum kwetu. Tunapaswa kuendelea na kiwango hiki cha juu na kupata pointi nyingi zaidi katika ligi."ARSENAL, MILAN, PORTO SAAFI

Goli lililofungwa na Mario Balotelli kuelekea mwishoni mwa mechi liliiokoa Manchester City isifungwe nyumbani katika mechi yao dhidi ya Borussia Dortmund na kuambualia sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Etihad jana.

Marco Reus aliifungia Dortmund bao la utangulizi lililoelekea kuwazamisha wenyeji kabla mpira uliopigwa na Sergio Aguerro haujagonga mkono wa Neven Subotic na refa kuwapa penati iliyofungwa kiufundi na Balotteli katika dakika za lala salama.

Matokeo hayo yaliifanya Man City iambulie pointi yake ya kwanza katika mechi mbili walizocheza na hivyo kushika nafasi ya tatu kwenye kundi lao la D, wakiachwa kwa pointi tano na vinara Real Madrid.

Arsenal walijiimarisha kileleni mwa kundi lao la B baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa mabao 3-1 dhidi ya
Olympiakos.

Magoli kutoka kwa Gervinho, Lukas Podolski na la ‘usiku’ kutoka kwa Aaron Ramsey ndiyo yaliyowapa ushindi Arsenal na kubaki kileleni mwa kundi lao baada ya kufikisha pointi sita, wakifuatiwa na Schalke wenye pointi nne.   

Goli la Souleymane Camara katika dakika ya mwisho liliipa Montpellier sare ya ugenini ya 2-2 dhidi ya Schalke na hivyo kuipa Arsenal uongozi wa pointi mbili zaidi katika kundi lao la B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Montpellier walipata bao la utangulizi kabla wenyeji hawajasawazisha kupitia Julian Draxler. Penati iliyofungwa na Klaas-Jan Huntelaar ilionekana kuwapa ushindi Schalke kabla Montpellier hawajasawazisha katika dakika ya mwisho kupitia kwa Camara na hivyo kuiacha Schalke ikibaki na pointi nne.

Porto walikwea kileleni mwa Kundi A baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya Paris St-Germain, ambapo goli hilo lilifungwa katika dakika ya 83 na mashambuliaji wao James Rodriguez.

Na goli la kujifunga kuelekea mwishoni mwa mechi kutoka kwa beki Tomas Hubocan kuliigharimu Zenit St Petersburg na kujikuta wakilala nyumbani kwa mabao 3-2 katika mechi yao dhyidi ya AC Milan.

No comments:

Post a Comment