Friday, October 5, 2012

LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA SITA


Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.

Jumapili (Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).
 

No comments:

Post a Comment