Wednesday, September 5, 2012

CHAMAKH AUGUA, ASHINDWA KUITUMIKIA MOROCCO

Marouane Chamakh

RABAT, Morocco
KUREJEA kwa Marouane Chamakh kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kumepata pigo kutokana na tatizo la kiafya la straika huyo, shirikisho la soka la Morocco limesema leo.

Straika huyo wa Arsenal ameitwa kuichezea timu hiyo ya kaskazini mwa Afrika katika mechi yao ya kwanza ya raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu kwa fainali Mataifa ya Afrika nchini Msumbiji Jumapili.

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuitwa tangu alipotemwa wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwanzoni mwa mwaka.

Shirikisho halikuweka wazi taarifa za undani za ugonjwa huo wa Chamakh. Nafasi yake imejazwa na mzaliwa wa Ufaransa, Abdelaziz Barrada wa klabu ya Granada ya Hispania.

No comments:

Post a Comment