Sunday, July 8, 2012

WEMA, JACQUELINE WOLPER WATOKA SARE

Hamna kupigana za uso mtaharibiana 'resepsheni'.... Refa John Chagu (katikati) akiwaalika Wema Sepetu (wa pili kulia) na Jacqueline Wolper (kushoto) waanze kuzichapa wakati wa pambano lao la hisani katika tamasha maalum la kuchangia Taasisi ya Elimu (ETA) kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali za sekondari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7, 2012. Nyota hao wa filamu nchini walitoka sare. Wengine pichani ni kocha wa Wema, Rashid Matumla (kulia) na kocha wa Wolper, Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo' (wa pili kushoto).

Wolper na Wema wakizichapa wakati wa pambano lao la hisani.

Nenda ukampe chembe-kidevu, lazima akae..... Wema akipata mawaidha kutoka kwa kocha wake Rashid Matumla wakati wa pambano lao la raundi mbili lililofanyika katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwaja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Sikukuu ya Sabasaba (Julai 7, 2012).

Diamond njoo unisaidie.... Wema (kulia) akielemewa na Jacqueline Wolper wakati wa pambano lao la hisani katika tamasha maalum la kuchangia Taasisi ya Elimu (ETA) kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali za sekondari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7, 2012. Wasanii hao wa filamu walitoka sare.


PICHA ZOTE: http://www.globalpublishers.info/

No comments:

Post a Comment