Wednesday, July 18, 2012

WAJUA BOTI ILIYOZAMA ILITENGENEZWA LINI? SOMA HAPA. NA PICHA ZAIDI.

Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika boti iliyozama leo. Hawa ni baadhi ya waliosalimika


Abiria waliookolewa kutoka katika boti iliyozama ya Skagit katika eneo la Chumbe Zanzibar leo.


Abiria aliyenusurika kutoka katika boti ya Skagit iliyozama leo

Abiria aliyenusurika katika boti iliyozama ya Skagit akifarijiwa na jamaa zake baada ya kuteremka katika boti iliyowaokoa.


Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona majeruhi waliookolewa katika boti iliyozama ya Skagit wakiteremka bandarini Zanzibar.



Askari wa vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya uokozi kwa abiria waliokuwa katika boti ya Skagit iliyozama Zanzibar leo.
Picha zote na Yussuf Simai Maelezo

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar Dk Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kuzama kwa Meli ya Skagit katika eneo la Chumbe Zanzibar.

Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama na meli ya Skagit leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akiwa katika eneo la bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi na miili ya waliozama Zanzibar leo

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika eneo la bandari leo

Majeruhi aliyeokolewa katika boti ya Skagit iliyozama leo

Majeruhi wakipatiwa mablanketi kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika boti ya Skagit leo


Dk Shein Afika Bandarini Malindi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na viongozi wakuu wa Serikali alipofika katika Ofisi za Shirika la Bandari, Malindi Unguja kupata taarifa sahihi za ajali ya kuzama kwa boti ya MV Skagit ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Mv Skagit katika Picha





Hizi ndizo boti za Mv Skagit ambazo kwa mara ya kwanza blog ya http://othmanmapara.blogspot.com/ iliripoti kuhusu ununuzi wake tarehe 19/02/2011 na hapa chini ndiyo maelezo yake

Vifaa vilivyonunuliwa kutoka Marekani - Washington State na moja ya kampuni za usafiri kwa Dola laki nne kwa zote mbili ambapo vitakapowasili vitatoa huduma za usafiri kati ya Zanzibar na Dar.
Boti hizi zilitengenezwa mwaka 1989 na kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 250 ziliwahi kuwekwa kwenye mtandao wa E bay kwa bei ya Dola laki tatu kila moja lakini hazikupata wateja. Zilipotengenezwa mwaka 1989 ziligharimu Dola milioni tano.






CHANZO: http://othmanmapara.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment