Friday, July 13, 2012

TUSKER, PORTS ZATUA KUKAMILISHA TIMU KOMBE LA KAGAME

Nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa akiinua kombe baada ya kukabidhiwa baada ya fainali ya Kombe la Kagame mwaka jana ambapo umeme ulikatika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kulazimisha timu hiyo kukabidhiwa taji lao gizani. Mwaka huu Nsajigwa, ambaye alikuwa shujaa wa timu hiyo, hatakuwepo kwa sababu ametemwa katika kikosi cha michuano hiyo na kocha mpya Mbelgiji Tom Saintfiet. Picha: Khalfani Said

TUSKER ya Kenya na Ports ya Djibouti zinawasili leo jioni kukamilisha idadi ya timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Mechi za kesho ni APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya Burundi.
 
Timu zote kutoka nje ya mazoezi zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo zitavitumia kwa mujibu wa ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makazi ya timu hizo na viwanja vya mazoezi ni kama ifuatavyo;
 
Timu:                   Uwanja wa mazoezi:              Accommodation:
APR (Rwanda)       Mabibo Hostel                         - Marriott Hotel (Mabibo External)
AS Vita (Congo)    University of Dar es Salaam     - Chichi Hotel (Kinondoni)
Atletico (Burundi) Mabibo Hostel                         - Lunch Time Hotel (Mabibo Hostel)
Azam (Tanzania)   Azam Complex                        - Azam Complex (Chamazi)
El Salam Wau (S. Sudan) Zanaki Sekondari           - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Mafunzo (Z’bar)    Kinesi                                     - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Ports (Djibouti)     Kinesi                                     - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Simba (Tanzania)  …………………….                         – Vina Hotel (Mabibo Makutano)
Tusker (Kenya)     Zanaki Sekondari                     - Rungwe Hotel (Kariakoo)
URA (Uganda)       Loyola                                     - Valentino Royal Hotel (Kariakoo)
Yanga (Tanzania)  ………………….                            – ……………………….

No comments:

Post a Comment