Tuesday, July 3, 2012

TIMU 10 TANZANIA KUCHEZA ROLLINGSTONE BURUNDI

TIMU 10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya Rollingstone kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu itafanyika Makamba nchini Burundi kuanzia Julai 7 mwaka huu.

Jumla ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa katika makundi sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda na Zanzibar.

Timu za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam, Bishop High School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting, Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life. 

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu zote zinatakiwa kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili kuthibitisha umri wao. Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu umri wa mchezaji yeyote.

Kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji 20 na viongozi watano ambao watagharamiwa na waandaaji kwa huduma za malazi na chakula kwa muda wote wa mashindano hayo yaliyoanzishwa miaka 13 iliyopita.

No comments:

Post a Comment