Saturday, July 7, 2012

Tetesi za usajili Jumamosi

TETESI ZA USAJILI

Robin van Persie

 

VAN PERSIE ATAKIWA MAN U, BARCA

MANCHESTER City watatuma maombi ya kutaka kumsajili straika wa Arsenal, Robin Van Persie, 28, kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15, lakini Barcelona na Paris Saint-Germain pia wanamuwania mchezaji huyo, ambaye ameamua hatasaini mkataba mpya.
Habari kamili: the Sun 


AC MILAN PIA WAMHITAJI RVP

VITA ya kumuwania Van Persie imeongezeka baada ya AC Milan kuingia katika mbio za kutaka kumsajili Mholanzi huyo.
Habari kamili: The Times (kwa kulipia) 


RVP ATATUPA UBINGWA ULAYA - KOLO TOURE

MANCHESTER City watatwaa kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kama Robin van Persie atatua Etihad Stadium, kwa mujibu wa beki wa City, Kolo Toure.
Habari kamili: Daily Telegraph 


SOL CAMPBELL: MKIMWAGA PESA RVP ATABAKI 
 
BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell, 37, ameiambia klabu yake ya zamani kwamba njia pekee ya kumbakisha Van Persie ni kutumia paundi milioni 100 katika kununua wachezaji wapya wa kiwango cha dunia.
Habari kamili: Daily Mirror 


VIONGOZI ARSENAL WATIA PAMBA MASIKIONI
 
MWENYEKITI wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema shutuma dhidi ya klabu hiyo inavyoendeshwa ni "upuuzi mtupu".
Habari kamili: the Guardian 
 

VIDIC KUREJEA MAPEMA
 
NAHODHA wa Manchester United, Nemanja Vidic, 30, anatumai kwamba atakuwa fiti kwa ajili ya mwanzo wa msimu baada ya kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza.
Habari kamili: Daily Mail 


ANELKA ATAKA KUREJEA ENGLAND

NICOLAS Anelka, 33, anapanga kurejea kwenye ligi kuu ya England baada ya mahusiano yake na Shanghai Shenhua kuwa mabaya, kutokana na kutofautiana na mashabiki.
Full story: Metro 

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMNASA STRAIKA WA ROMA

KOCHA Brendan Rodgers anakaribia kumsajili straika wa Roma, Fabio Borini, 21, ili awe mchezaji wa kwanza kumsajili tangu akabidhiwe mikoba ya kuifundisha klabu hiyo ya Anfield.
Habari kamili: Daily Telegraph 
Roma's Fabio Borini
Fabio Borini aliisaidia Swansea kupanda daraja la Ligi Kuu wakati alipoichezea kwa mkopo akitokea Chelsea


DEFOE UKITAKA ONDOKA 

STRAIKA wa timu ya taifa ya England, Jermain Defoe, 29, ameambiwa na kocha mpya Andre Villas-Boas kwamba anaweza kuondoka Tottenham.
HAbari kamili: Daily Mail MODRIC AKARIBIA KUTUA REAL MADRID

LUKA Modric, 26, anakaribia kuafiki dili la uhamisho litakalogharimu paundi milioni 28 ili kuhama kutoka White Hart Lane na kutua Real Madrid.
Habari kamili: talkSPORT 


NEWCASTLE YAMKATAA "FUNDI" HOILETT
 
NEWCASTLE imekataa fursa ya kumsajili winga 'fundi' wa kuwapunguza mabeki Junior Hoilett, 22, kutoka Blackburn, lakini wanakaribia kumsajili mchezaji yosso wa timu ya taifa ya vijana ya Australia ya U-20,  Curtis Good,  19, kutoka Melbourne Heat.
Habari kamili: Newcastle Chronicle 


No comments:

Post a Comment