Saturday, July 7, 2012

TAZAMA MAFURIKO YANAVYOENDELEA KUANGAMIZA WATU URUSI


Ni balaa....! Baadhi ya magari yakisombwa na mfuriko hayo nchini Urusi leo.
KRASNODAR, Urusi
Takriban watu 87 wamekufa baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kusababisha mafuriko kusini mwa Urusi katika eneo la Krasnodar, maafisa wamesema leo.

Mafuriko hayo ambayo hayakuwa yametabiriwa na wataalam wa hali ya hewa, yaliibuka ghafla usiku wa kuamkia leo kuwakuta watu wengi wakiwa katika hali ya kutojua la kufanya.

Vikosi vya uokoaji kutoka katika jijila Moscow vimepelekwa kwa ndege na helikopta katika eneo hilo. Picha za luninga zimekuwa zikionyesha mamia ya watu wakigombania kukwea kwenye mapaa ya nyumba kwa nia ya kujiokoa.

Mbali na kuua makumi ya watu na kujeruhi, mafuriko hayo yenye nguvu za ajabu pia yamekuwa yakisomba magari na kubomoa miundomboinu ya barabara na makazi ya watu takriban 13,000.

"Hadi sasa hakuna umeme na maduka yamefungwa. Maelfu ya watu wamepoteza kila kitu na sasa wanahaha kuokoa maisha yao,” alisema mmoja wa mashuhuda."

No comments:

Post a Comment