Saturday, July 14, 2012

TATIZO LA FABRICE MUAMBA LAMUANGUSHA MUIGIZAJI MAARUFU

Michael Clarke Duncan

MUIGIZAJI maarufu wa Hollywood, Michael Clarke Duncan, yuko katika chumba chenye uangalizi maalum katika hospitali ya Los Angeles baada ya moyo wake kusimama kufanya kazi (cardiac arrest) asubuhi ya jana ... na pengine angekufa kama sio kitendo cha haraka kilichofanywa na rafikiye wa kike, Omarosa Manigault.

Omarosa alibaini kwamba muigizaji huyo wa filamu ya "Green Mile" alikuwa amepigwa na tatizo hilo la moyo kiacha kusukuma damu majira ya saa 8:00 usiku.

Mwanadada huyo Omarosa alimsaidia mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 54 na haraka akawahishwa katika hospitali ya jirani ambako alipelekwa ICU.

Duncan akiwa na rafikiye wa kike, Omarosa Manigault

Vyanzo vimesema kuwa moyo wa Duncan sasa unafanya kazi na Omarosa yuko pembeni yake. Madaktari wanamfanyia vipimo kubaini sababu za moyo wake kusimama.

Mtoa habari wa muigizaji huyo alisema: "Kwa mujibu wa madaktari, Michael Clarke Duncan alipatwa na tatizo hilo ambalo linaweza kumtokea mtu yeyote. Hivi sasa anaendelea vyema na anasubiria kupona kikamilifu."Duncan

Kabla ya kuwa muigizaji, Duncan alikuwa baunsa wa wasanii maarufu kama Will Smith, Martin Lawrence, Jamie Foxx, LL Cool J, na Notorious B.I.G. Wakati Notorious B.I.G. akiuawa mwaka 1997, rafiki yake alimkingia Duncan asiuawe pia. Hii ndiyo iliyokuwa sababu ya Duncan kuacha kazi hiyo. 

Aliingia katika filamu mwaka 1998 kwa ushawishi wa muigizaji maarufu Bruce Willis na tangu wakati huo amecheza filamu nyingi kama "The Whole Nine Yards," "Planet of the Apes," "The Scorpion King" (ambayo alicheza pamoja na rafiki yake, The Rock), "The Island" na "Daredevil" ambayo aliigiza kama Wilson Fisk a.k.a The Kingpin.
Duncan

Mwili mkubwa wa Duncan --- ambaye ana urefu wa futi 6 na inchi 5 (196 cm) na uzito wa Kg. 142 — ulimsaidia kupata dili za ubaunsa katika klabu za usiku za mjini Chicago.


Kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba alianguka uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Tottenham, baada ya moyo wake kuacha kufanya kazi, tukio lililosababisha kuvunjwa kwa mechi hiyo. Alizinduka akiwa hospitalini huku akielezewa na madaktari kwamba alifariki kwa saa 72.
 

No comments:

Post a Comment