Saturday, July 7, 2012

TAMASHA LA FILAMU TANGA LILIVYOFUNGWA

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah akimkabidhi zawadi mtoto Omary Juma aliyeibuka mshindi wa jumla wa kucheza muziki katika muendelezo wa Tamasha la Wazi la Filamu nchini lililokuwa limedhaminiwa na Kampuni hiyo kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt mjini Tanga.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Wazi la Filamu ambalo limefika tamati jioni ya jana kwenye Viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.

Kiduku ndio mtindo wetu...... bhaaaaaaaas. Watoto wa mjini Tanga wakichuana kudansi wakati wa sherehe ya kufunga tamasha la filamu lililodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt.

No comments:

Post a Comment