Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea |
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)
imeanza uchunguzi mkali dhidi ya vigogo wanaodaiwa kuficha Uswisi mabilioni ya
fedha walizopata kwa njia haramu.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George
Mkuchika, ametoa taarifa hizo Bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimisha mjadala kuhusu makadirio na matumizi
ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Mkuchika alisema kuwa hadi sasa, tayari TAKUKURU imeanza kushughulikia
tuhuma hizo kwa kuwasiliana na watu wa Uswisi ili mwishowe undani wa jambo hilo
ufahamike na hatua stahili kuchukuliwa.
Awali, wabunge mbalimbali waliitaka Serikali kufanya
uchunguzi juu ya madai kwamba wapo vigogo mbalimbali serikalini
walijilimbikizia zaidi ya Sh. bilioni 300 nchini Uswisi na kwamba, ‘mihela’
hiyo imepatikana kwa njia zisizo halali, zikiwemo zilizopatikana kupitia baadhi
ya mikataba ya utafutaji mafuta na gesi ambayo mwishowe italigharimu taifa.
No comments:
Post a Comment