Monday, July 2, 2012

SUGU AIBUA UPYA SOO LA DKT. ULIMBOKA BUNGENI, AFANANISHA TUKIO HILO NA UNYAMA WA 'JANJAWEED'

Sugu

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi (CHADEMA) ameibua upya bungeni sakata la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Steven Ulimboka kwa kutaka tume huru iundwe mara moja ili kuchunguza ukweli wa tukio hilo.
Sugu alisema Serikali yenyewe haiaminiki kuhusiana na sakata hilo na hivyo kuna umuhimu wa kuwa na tume huru.

Sugu aliibua sakata hilo jioni hii (dakika chache) zilizopita wakati akichangia akichangia hoja ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma); akisisitiza kuwa suala hilo ni muhimu kufanyiwa kazi kwa minajili ya kutunza amani na utulivu katika nchi.

Hata hivyo, Sugu aliipata wakati mgumu kutoka kiti cha mwenyekiti wa mkutano huo, Sylvester Mabuma, baada ya kufananisha sakata la kutekwa  na kushambuliwa Ulimboka na vitendo vilivyokuwa vikifanywa na kikundi cha 'Janjaweed' cha Sudan ambacho kilikuwa kikitesa na kuwaua wananchi nchini humo.

Kabla ya kuzua soo hilo, Sugu alisema kwamba anafahamu kuwa sakata la mgomo wa madaktari liko mahakamani, lakini yeye anachozungumzia ni suala la kutekwa kwa Ulimboka ambalo lenyewe haliko mahakamani na hivyo hakuna kikwazo katika kulijadili.

Alisisitiza kwamba iundwe tume kama ya 'Dk. Mwakyembe" (wakati wa sakata la Richmond) ili ukweli wa kila kilichotokea kwa Ulimboka ufahamike na wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.



No comments:

Post a Comment