Tuesday, July 3, 2012

SAMIR NASRI, BEN ARFA WASHITAKIWA UFARANSA

Samir Nasri

Yann Mvila
Hatem Ben Arfa (kushoto) na Phillipe Mexes wakiwa katika mazoezi ya timu yaoya taifa ya Ufaransa. 

Jeremy Menez
PARIS, Ufaransa
SHIRIKISHO la Soka la Ufaransa (FFF) limefungua mashtaka dhidi ya wachezaji Samir Nasri, Hatem Ben Arfa, Jeremy Menez na Yann Mvila wa timu yao ya taifa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye fainali za Euro 2012, rais wa shirikisho hilo, Noel Le Graet amesema leo.

"Hatem Ben Arfa, Yann Mvila, Samir Nasri na Jeremy Menez wameitwa mbele ya kamati ya nidhamu," Le Graet aliuambia mkutano na waandishi wa habari leo.

Ufaransa walitolewa katika hatua ya robo fainali na waliokuja kuwa mabingwa, timu ya taifa ya Hispania na hivi sasa hawana kocha baada ya Laurent Blanc kukataa kuongeza mkataba wake.


No comments:

Post a Comment