Monday, July 16, 2012

CRISTIANO RONALDO SASA PASUA KICHWA REAL MADRID


*MSHAHARA WAKE MPYA KUIGHARIMU REAL BIL.44/-

Kwa matanuzi kama haya, Ronaldo lazima adai mkwanja mnene si wa kitoto. Hapa anakula maraha na demu wake Irina Shayk, mtoto wake wa kiume na wapambe kibao ndani ya boti ya bei mbaya kwenye fukwe za St. Tropez, Ufaransa Julai 3, 2012.
.
Si unaouona mwili ulivyojengeka kispoti... hapa ni misosi ya mpangilio na mazoezi makali. Kwanini asidai mwakanja mnene?

Kuwa na demu mkali kama Irina Shayk, anayekupa maraha kwa kukulalia mgongoni kunahitaji mkwanja ati... nd'o mana Ronaldo anaihenyesha Real kwa kutaka salary ndefu si ya kitoto.Kidali poh...! Ronaldo na demu wake Irina Shayk wakifaidi maraha kwenye fukwe za St. Tropez, Ufaransa Julai 3, 2012.

Wanasikia raha au au utamu?

Niache hukoo...! Ronadlo na kimwana wake Irina wakicheza kwenye fukwe za St. Tropez, Ufaransa. 

Ronaldo na demu wake

Hapa ni Ronaldo, kimwana wake Irina, mtoto wake na wapambe kibao wakiendelea kula maraha katika fukwe za St. Tropez. Bila kulipwa mkwanja mrefu atamudu mambo haya?

Ronaldo, mtoto wake na wapambe wakiendelea kuponda maraha.
Ronaldo (kulia) na wachezaji wenzake wa Real wakizunguka na kombe katika mitaa ya jiji la Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania msimu uliopita. Straika huyu aliibeba sana Real, akifunga mabao 46 katika mechi 38 za La Liga na kuifanya klabu hiyo iandike rekodi mpya Hispania kwa kufikisha magoli 121 na pia kuweka rekodi ya kufikisha pointi 100 katika ligi. Kwanini asidai mkwanja mrefu?   
MADRID, Hispania
KUTUPWA kwa ‘Sheria ya David Beckham' kumewafanya wachezaji nyota nchini Hispania sasa wakitozwa kodi kama watu wengine wanaoingiza vipato vikubwa nchini humo.

Ronaldo anataka kusainiwa kwa mkataba mpya utakaomhakikishia mshahara wa Euro milioni 15 kwa mwaka, ambao unamaanisha kuwa baada ya kutupwa kwa sheria ya Beckham, Real Madrid sasa watalazimika kumlipa mshahara ‘kufuru’ wa Euro milioni 23  (Sh. bilioni 44) kwa mwaka ili nyota huyo wa zamani wa Manchester United aendelee kuichezea timu hiyo.

Hata hivi sasa, ambapo anapokea mshahara wa Euro milioni 9.5 (Sh. bilioni 18) kwa mwaka, Ronaldo atailazimu Real kumlipa Euro milioni 12 (Sh. Bilioni 23) kwa mwaka ili kufidia pengo la makato linalotokana na sheria mpya ya kodi nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment