Sunday, July 15, 2012

Roma apagawisha Copa Coca Cola

Roma Mkatoliki akipagawisha baada ya fainali ya Copa Coca Cola kwenye Uwanja wa Karume leo.


Na Sanula Athanas
NYOTA wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki leo jioni amewapagawisha kwa ‘michano’ ya hatari watu waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya fainali ya michano ya Copa Coca Cola kati ya Mwanza na Morogoro.

Roma, Mshindi wa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Hip Hop 2011, alianza kuonesha makali yake muda mfupi baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ambayo Morogoro walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Katika onesho hilo, Roma alikuwa ameambatana na wakali wengine akiwamo Darasa aliyeshirikiana naye katika kulipamba jukwaa.

Msanii huyo kutoka mkoani Tanga alikuwa ‘akichana mistari’ na kucheza huku akigawa zawadi za fulana kwa mashabiki wake na watu mbalimbali waliokuwa wamefurika kushuhudia onesho hilo.
 

No comments:

Post a Comment