Saturday, July 14, 2012

RIO FERDINAND: MADOGO WANATAKA NAMBA YANGU MAN UTD

Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand  na dereva wa magari ya Formula One, Lewis Hamilton (juu) wakihudhuria uzinduzi wa mashindano ya London Grand Prix mjini London, England Juni 28, 2012.

BEKI wa Manchester United, Rio Ferdinand, ana hamu kubwa ya kuona msimu mpya wa Ligi kuu ya England unaanza.

Mapumziko ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 ya mwezi Juni yalipata pigo wakati alipoachwa isaivyotarajiwa nje ya kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoenda kwenye fainali za Euro 2012.

Alibainisha: "Nimekuwa na likizo ndefu mno. Niko tayari kwa asilimia 100 kuweka kila kitu kwenye soka hivi sasa.

Rio Ferdinand

Rio Ferdinand akijifua

"Unapoona ratiba imetoka unaanza kuwaza mazoezi.

"Naelekea ukingoni mwa zama zangu za kucheza soka hivyo nahitaji kurejea nikiwa fiti kwa kadri niwezavyo ili kula sahani moja na vijana wadogo."

No comments:

Post a Comment