SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mjumbe wake wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa kilichotokea Julai 5 mwaka
huu kutokana na maradhi.
ACP
Semlangwa ambaye alizikwa juzi (Julai 6 mwaka huu) katika Kijiji cha
Gumba, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani alitoa mchango mkubwa akiwa
mjumbe wa Kamati hiyo inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu
Alfred Tibaigana.
Msiba
huo ni pigo kwa familia ya ACP Semlangwa, TFF na familia ya mpira wa
miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa
shirikisho akiwa mjumbe wa kamati hiyo.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu ACP Semlangwa, jamaa na marafiki na
kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia
TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi
zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu ACP Shabani Semlangwa mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment