Saturday, July 14, 2012

ONA BALAA LA NICKI MINAJ

Nicki Minaj akiwa katika kipindi cha “The Tonight Show with Jay Leno” jana

Nicki Minaj akirekodi video ya 'Pound the Alarm' nyumbani kwao Trinidad.

Nicki Minaj akirekodi video ya 'Pound the Alarm' nyumbani kwao Trinidad.

Nicki Minaj akirekodi video ya 'Pound the Alarm' nyumbani kwao Trinidad.
Rapa Nicki Minaj (kulia) akipokea tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Hip Hop kutoka kwa rapa Busta Rhymes wakati wa tamasha la Tuzo za BET 2012kwenye Ukumbi wa Shrine Auditorium mjini Los Angeles, California Julai 1, 2012.
Nicki Minaj (kushoto) akipozi Busta Rhymes wakati wa tamasha la Tuzo za BET 2012kwenye Ukumbi wa Shrine Auditorium mjini Los Angeles, California Julai 1, 2012.

Nicki Minaj (kushoto) akipozi Busta Rhymes wakati wa tamasha la Tuzo za BET 2012kwenye Ukumbi wa Shrine Auditorium mjini Los Angeles, California Julai 1, 2012.

Nicki Minaj alivamia steji ya kipindi cha televisheni cha “The Tonight Show with Jay Leno” jana. Akiwa amevalia "kibodesuti" chenye rangi inayomfanya aonekane kama hajavaa nguo (mcheki pichani), kimwana huyo alitumbuiza kwa wimbo wake mpya "Pound the Alarm" na kisha akakaa kwenye kochi kwa ajili ya mahojiano na Jay Leno.

Wakati wa mahojiano, alikumbushia kuhusu kazi yake ya zamani ya mhudumu wa mgahawa. "Sikutaka kuendelea kukaa pale na hata wateja walibaini," alisema Nicki. "Daima wanaagiza mikate mno. Hilo lilikuwa likinikera. tafadhali mkienda pale Red Lobster, acheni kuagiza mikate ya ziada."

Rapa huyo wa lebo ya Young Money, alivaa vazi kama hilo ambalo huvaliwa katika matamasha ya Carnival yanayofahamika pia kama matamasha ya Samba wakati akirekodi video ya wimbo huo mpya wa "Pound the Alarm" nyumbani kwao Trinidad wiki iliyopita. Video hiyo bado haijatoka.

Nicki ataanza ziara yake inayokwenda kwa jina la "Pink Friday" Jumatatu mjini Chicago akishirikiana na mgeni mwalikwa rapa 2 Chainz.

No comments:

Post a Comment