Tuesday, July 17, 2012

MATUMLA APIGWA TKO RAUNDI YA 4 UJERUMANI

Refa wa ngumi Jean Piere (katikati) akimuinua mkono bondia Benjamin Simon a.k.a Iron Ben kumtangaza mshindi wa pambano lake dhidi ya Rashid Matumla 'Snake Man' kwenye Ukumbi wa Universal, Ujerumani usiku wa kuamkia Jumapili.

Bondia Benjamin Simon 'Iron Ben' wa Ujerumani akipozi na Rashid Matumla 'Snake Man' wa Tanzania kabla ya pambano lao lililofanyika Jumamosi usiku. 

Na Mwandishi Wetu
BONDIA gwiji nchini Tanzania, Rashid Matumla 'Snake Man' amepigwa kwa Technical Knock-out ya raundi ya nne dhidi ya bondia Benjamin Simon a.k.a 'Iron Ben' wa Ujerumani katika pambano lao la uzani wa Supermiddle lililokuwa kuwania mkanda wa IBF kwenye Ukumbi wa Universal, Ujerumani usiku wa kuamkia Jumapili.

Pambano hilo la raundi 12 lilikuwa ni la pili baina ya mabondia hao baada ya Matumla kupigwa kwa pointi katika pambano lao la awali lililofanyika Febriari 6, 2010 Boxtempel, Ujerumani.

Mratibu wa pambano hilo, Ali Bakari 'Champion' wa Champion Sports Promotions ya Buguruni jijini Dar es Salaam akishirikiana na African Camp Promotion ya Kenya chini ya mkurugenzi wake, Thomas Mutua, aliiambia STRAIKA kuwa Matumla atarejea leo kupitia Nairobi.
 
Matumla aliondoka nchini Julai 10 kwa kupitia Nairobi, Kenya kwa ajili ya pambano hilo la usiku wa Jumamosi Julai 14.

Siku mbili kabla ya matumla kupaa kwenda Ujerumani kuwania taji hilo, alikuwepo kwenye Tamasha la Matumaini, ambapo alikuwa mwalimu wa ngumi wa muigizaji Wema Sepetu kwa ajili ya pambano lake la hisani dhidi ya muigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper.

No comments:

Post a Comment