Sunday, July 15, 2012

MUINGEREZA AMIR KHAN ADUNDWA 'KO' RAUNDI YA 4

KIJANA WA KIARABU 'ALAMBA SAKAFU' MARA 3

Danny Garcia wa Marekani akishangilia ushindi wake wa raundi ya nne dhidi ya Amir Khan wa Uingereza katika pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS

Danny Garcia wa Marekani akishangilia ushindi wake wa raundi ya nne dhidi ya Amir Khan wa Uingereza katika pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha:REUTERS
Amir Khan wa Uingereza akitibiwa baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya bingwa wa WBC, Danny Garcia wa Marekani katika pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS
Bingwa wa WBC, Danny Garcia (kushoto) akimchapa Amir Khan ngumi iliyompeleka chini Khan wakati wa pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS

Bingwa wa WBC, Danny Garcia (kushoto) akishangilia na memba wa kambi yake na bondia Bernard Hopkins (kulia) baada ya kumdunda Amir Khan katika raundi ya 4 wakati wa pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS
Danny Garcia (kushoto) akimshuhudia Amir Khan akienda sakafuni wakati wa pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS

Mimi ndio mimi... Danny Garcia akishangilia

Refa Kenny Bayless (kushoto) akimzuia Amir Khan wa Uingereza baada ya kuangushwa chini katika raundi ya nne na kuhitimisha mchezo wakati wa pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS

Refa wa ngumi Kenny Bayless (kulia) akimhesabia Amir Khan wa Uingereza baada ya kuangushwa chini na Danny Garcia wa Marekani kabla ya kuvunja pambano katika raundi ya nne  la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS

Halua halua... inuka nione. Amir Khan akijikongoja kunyanyuka kutoka 'sakafuni' baada ya kudondoshwa na Danny Garcia huku refa Kenny Bayless akimpelekea Garcia kwenye kona wakati wa pambano lao la ubingwa wa mataji ya WBC/WBA light-welterweight kwenye ukumbi wa Mandalay Bay Events Center mjini Las Vegas, Nevada leo asubuhi. Picha: REUTERS
Upper cut chembe kidevu, lazima ukae... Amir Khan akiwa amekalishwa. Chezea Gacia wewe?

LAS VEGAS, Marekani
MMAREKANI Danny Garcia amempiga Muingereza Amir Khan katika raundi ya nne na kuongeza taji la WBA la uzito wa light-welterweight kwenye taji lake WBC super-lightweight mjini Las Vegas katika pambano lililofanyika leo asubuhi.

Khan, mwenye rekodi ya kushinda mapambano 26 (18 kwa KO) na kupigwa matatu, alionekana kutawala mapema, mikono yenye kasi zaidi wakati alipomchapa ngumi mfululizo za mkono wa kulia kabla ya kumchana jicho Garcia kwa ngumi ya kushoto.

Garcia aliendelea kujilinda mno na kimafanikio, na katika raundi ya tatu akanza kurusha ngumi nzito kwenye mwili wa Khan na karibu na mwisho wa raundi hiyo alimkandamiza ngumi kali Khan iliyomfanya aangukie makalio.

Muingireza huyo alijikongoja kunyanyuka, lakini baada ya kusimama huku miguu ikiwa imetepeta kengele ikalia na kumuoka.

Garcia alimuangusha Khan tena mwanzoni mwa raundi ya nne kwa ngumi ya mkono wa kulia na wakati akijaribu kurejea mchezoni, Garcia alimuandama, akimtwanga ngumi nzito mfululizo.

Mkono wa kushoto ukampeleka Khan chini tena, na ingawa aliweza kunyanyuka kabla hajamaliza kuhesabiwa, refa Kenny Bayless alimaliza pambano ingawa Muingereza huyo alidhani kwamba pambano lilisimamishwa mapema mno.

"Nilishangazwa na refa kusimamisha pambano," alisema. "Nilidhani angetuacha tuendelee. Akili yangu ilikuwa iko poa, na nilidhani miguu yangu ilikuwa 'okay'.

"(Lakini) haikuwa siku yangu. Namheshimu Danny. Alikuwa akijibu vizuri sana mashambulizi yangu. Nilifanya makosa kidogo na alitumia nafasi hiyo na akanipata."

Garcia alisema aliona kwamba Muingereza huyo alimdharau.

"Tulijua kwamba Khan angekuja kwa kasi kwa sababu alidhani kwamba sina nguvu," alisema Garcia ambaye ameboresha rekodi yake na kuwa 24-0 (15 kwa KO).

"Lakini nilisubiri na kisha nikamuandama na nikatumia kasi na nguvu nilizonazo. na ikafanikiwa."

Kipigo cha Khan kilikuwa cha pili mfululizo baada ya kupoteza mataji yake ya WBA na IBF kwa pointi dhidi ya Lamont Peterson Desemba mwaka jana.

Hata hivyo, Peterson alibainika kutumia dawa zinazokatazwa michezoni, ambazo alikiri kuzitumia kabla ya kupambana na Khan, na WBA wakamrejeshea Khan ubingwa wake wa dunia Alhamisi.

No comments:

Post a Comment