Saturday, July 14, 2012

MRUDISHIENI JOHN TERRY UNAHODHA ENGLAND

John Terry akitoka mahakamani baada ya kufutiwa mashitaka ya kumbagua Anton Ferdinand

GWIJI wa Arsenal, Kenny Sansom amesema nahodha wa Chelsea, John Terry anapaswa kurejeshewa kitambaa chake cha unahodha wa timu ya taifa ya England baada ya kufutiwa mashitaka ya ubaguzi wa rangi.

Sansom, ambaye aliichezea timu ya taifa ya England mara 86, anaona kwamba kocha Roy Hodgson anapaswa kumrejeshea unahodha wa taifa beki huyo wa Chelsea.

Beki huyo wa pembeni wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Arsenal aliliambia gazeti la The Sun: "Terry ni nahodha mzuri sana, tukio limetokea na sasa limepita.

"Wanamheshimu katika chumba cha kuvalia."

Terry alivuliwa unahodha wa timu ya taifa kufuatia tuhuma za kumtamkia maneno ya kibaguzi beki wa QPR, Anton Ferdinand, kitendo ambacho kilipingwa na kocha wa wakati huo wa timu ya taifa Fabio Capello, ambaye kutokana na jambo hilo alijiuzulu huku akimtetea beki huyo akisema: "Terry hapaswi kuonwa mwenye hatia hadi mahakama itakapoamua."

Kufuatia hukumu iliyotolewa jana ya kumfutia Terry mashitaka yote ya ubaguzi, Capello ameelezea furaha yake.

Kwa kuacha kazi, Capello alipoteza ajira iliyokuwa ikimuingiza paundi milioni 6 (sawa na Sh. bilioni 14.5) kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment