Sunday, July 15, 2012

MORO MABINGWA COPA COCA COLA 2012


Morogoro wakishangilia ubingwa wa Copa Coca Cola baada ya kuwafunga Mwanza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sanula Athanas.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akipokea kombe la ubingwa wa michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Copa Coca Cola, kutoka kwa nahodha wa timu ya mkoa wake baada ya kuwafunga Mwanza 1-0 katika fainali kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Picha: Sanula Athanas
 
Nahodha wa timu ya mkoa wa Morogoro akinyanyua kombe la ubingwa wa Copa Coca Cola baada ya kukabidhiwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Leodegar Tenga (mwenye shati jeupe).Mexime we mkali... Wachezaji wa timu ya vijana ya mkoa wa Morogoro wakimbeba kocha wao Mecky Mexime baada ya kuwaongoza kutwaa ubingwa wa Copa Coca Cola leo. Picha: Sanula Athanas 


Roma Mkatoliki akipagawisha baada ya fainali ya Copa Coca Cola kwenye Uwanja wa Karume leo.


Mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano ya Copa Coca Cola, Shiza Kichuya akipokea mfano wa hundi ya Sh. 750,000 alizozawadiwa baada ya fainali hizo leo.
 
Tuzo ya nidhamu ni kwa timu ya Tanga
 
Mshindi wa tuzo ya Kocha Bora kutoka Tanga 


Mshindi wa tuzo ya Mfungaji Bora

 Mashabiki walipendeza

Kikatuni (Mascot) nacho kilikuwepo kupamba fainali leo. Picha: Sanula Athanas  


Twende sasa... ni soka na muziki.

Shughuli yenyewe ilivyokuwa. 

Na Sanula Athanas
TIMU ya mkoa wa Morogoro leo imetwaa ubingwa wa michuano ya sita ya Copa Cocacola ya vijana wa umri chini ya miaka 17 baada ya kuifunga timu ya Mwanza kwa goli 1-0 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.


Goli la ushindi lilifungwa na Salum Ramadhani katika dakika ya 36 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Mwanza.


Kwa ushindi huo, Morogoro walitwaa kombe walilokabidhiwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodegar Tenga, ambaye alikuwa ameambatana na wasaka vipaji wa shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), Juera Nepfer ambaye ni mkuu wa elimu na maendeleo ya kiufundi kutoka Uswisi na Govinden Thondoo (Afisa wa Maendeleo ya Ufundi wa FIFA). Walipata pia zawadi ya kwanza ya Sh. milioni 8.


Washindi wa pili Mwanza walipata Sh. milioni 4.5, wakati Temeke walioibuka washindi wa tatu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanga walipata Sh. milioni 3.2. Tanga walipata Sh. milioni 1.5 kama timu yenye nidhamu.


Shiza Kichuya kutoka Morogoro aliibuka mchezaji bora wa michuano, Liston Hiyari (Mwamuzi Bora), Shukuru Mohammad wa Temeke (kipa bora), ambao kila mmoja walizawadiwa Sh. 750,000.
Kocha wa mabingwa wapya Morogoro, Mecky Mexime, ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', alisema mechi ilikuwa ngumu.


"Licha ya kwamba tuliwafunga hawa Mwanza 6-0 katika hatua ya makundi, fainali ni fainali tu, wamekuwa wagumu sana leo, lakini tunashukuru tumeshinda," alisema Mexime ambaye alikuwa nahodha wa Stars enzi za Marcio Maximo. 


Kocha wa msaidizi wa Mwanza, Mustapha Mtoro, alisema amewalaumu vijana wake kwamba walipata nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia.

No comments:

Post a Comment