Wednesday, July 11, 2012

MKE AMBURUZA KORTINI DK. SLAA AKIPINGA ASIMUOE JOSEPHINE MUSHUMBUZI


*ADAI FIDIA MIL.550, NDOA ILIPANGWA JUMAMOSI IJAYO

Dk. Slaa
Bi. Josephine Mushumbuzi
Dk. Slaa akiwa jukwaani na Josephine Mushumbuzi
Hapa Dk. Slaa (kulia) akiwa na Rose Kamili
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili, ametinga katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupinga ndoa iliyopangwa kufungwa Jumamosi ijayo (Julai 21) wilayani Karatu mkoa wa Manyara kati ya Bi. Josephine Mushumbuzi na aliyekuwa mumewe ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.

Rose ameomba pia kulipwa na wawili hao jumla ya Sh. Milioni 550, ikiwa ni fidia ya kuvurugiwa ndoa yake (na Dk. Slaa) na kwamba katika malipo ya fidia hiyo, Dk.Slaa amlipe Sh. milioni 50 na Josephine Sh. milioni 500.  

Wakili Joseph Thadayo ndiye aliyewasilisha maombi hayo kwa niaba ya Rose na kesi kupata usajili namba 4/2012, huku Jaji Laurence Kaduli akipangwa kuisikiliza.

Rose anadai kuwa Dk. Slaa ni mume wake halali tangu mwaka 1985. Anasema kuwa Juni 18, 1987, alizaa mtoto wa kwanza na Dk. Slaa waliyemwita Elimiliana Slaa na Septemba 23, 1988, wakapata mtoto wao wa pili waliyemwita Linus Slaa.

Alisema kuwa hata hati zao za kusafiria zilionyesha kuwa wao ni mke na mume na kwamba, katika kipindi cha kuishi pamoja, walichuma vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyumba mbili za kuishi, moja iko Sinza jijini Dar es Salaam, namba 609 Block E na nyingine katika Kijiji cha Gongali wilayani Karatu, iliyojengwa mwaka 2005.

Rose anadai kuwa uhusiano wa ndoa yao ulianza kuyumba mwaka 2009 baada ya mumewe huyo kuanza mahusiano na Mushumbusi ambapo tangu wakati huo amekuwa hatoi matunzo kwa familia yao, ikiwa ni pamoja na kutowahudumia kwa mavazi na chakula.

Rose ametaka Mahakama Kuu imuamuru Dk.Slaa ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza kumlipa fidia ya Sh. Milioni 50 na mlalamikiwa wa pili amlipe milioni 500, na kwamba wawili hao (Dk. Slaa na Josephine) wasiruhusiwe kufunga ndoa ya aina yoyote.
 


No comments:

Post a Comment