Monday, July 16, 2012

DROGBA, MESSI, RONALDO, ROONEY, VAN PERSIE WAWANIA TUZO MWANASOKA BORA UEFA

Ronaldo (kushoto) na Alonso wa Real Madrid wote wametajwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa UEFA

Fabregas (kushoto) na Lionel Messi wa Barcelona wote wanawania tuzo ya mwanasoka bora wa UEFA.
Wayne Rooney wa Manchester United
Robin van Persie (Arsenal)
Didier Drogba akiwa na Kombe la UEFA la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

LIONEL Messi, Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney na Robin van Persie ni miongoni mwa majina ya wachezaji 32 waliotajwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya UEFA ya Mwanasoka Bora wa Ulaya.
Orodha hiyo inajumuisha wachezaji 13 kutoka katika ligi kuu ya England, huku watano kati ya hao wakitokea Manchester City.

Ligi ya Hispania imetoa wachezaji 12, huku wachezaji 7 wakiwa ni wa Real Madrid, wanne Barcelona na mmoja wa Atletico Madrid.

Orodha hiyo imetokana na mwandishi wa habari mmoja aliyechaguliwa kutoka katika kila nchi mwanachama wa UEFA ambao walipigia kura majina ya wachezaji wao watano bora.

Tuzo hizo za UEFA zitafanyika Agosti 30 mjini Monaco.

Orodha kamili ni hii:

Aguero (Manchester City), Y Toure (Manchester City), Silva (Manchester City),  Hart (Manchester City), Kompany (Manchester City), Balotelli (Manchester City), Casillas (Real Madrid), Coentrao (Real Madrid), Xabi Alonso (Real Madrid), Ozil (Real Madrid), Pepe (Real Madrid), Ramos (Real Madrid), Ronaldo (Real Madrid), Cech (Chelsea), Lampard (Chelsea), Torres (Chelsea), Drogba (Shanghai Shenhua), Davies (Bangor City), Fabregas (Barcelona), Iniesta (Barcelona), Xavi (Barcelona), Messi (Barcelona), Falcao (Atletico Madrid), Ibrahimovic (AC Milan), Rooney (Manchester Utd), Kagawa (Manchester Utd), Blaszczykowski (Borussia Dortmund), Modric (Tottenham), Pirlo (Juventus), Buffon (Juventus), Raul (Al-Sadd Sports Club), Van Persie (Arsenal).

No comments:

Post a Comment