Sunday, July 8, 2012

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI YALIVYOPAMBA MOTO MWANZA

Wasanii wa kikundi cha Bujora kilichoibuka na ubingwa wa Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi wakishambulia jukwaa wakati wa fainali za mashindano hayo ya mjini Mwanza yaliyoshirikisha vikundi kutoka wilaya za Nyamagana, Ukerewe na Sengerema. Bujora walizawadiwa Sh.600.000 kwa kuibuka washindi wa mchuano huo ulioandaliwa na bia ya Balimi.

Wasanii wa kikundi cha kutoka Ukerewe wakifanya mambo wakati wa Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Mashindano hayo yamedhaminiwa na bia ya Balimi.

Majaji wa Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi wakifuatilia kwa makini mpambano.

Sylvester Ngabula (kushoto) ambaye ni Katibu Mkuu wa Kikundi cha Bujora akipokea kiasi cha Sh.600,000 kutoka kwa meneja wa bia ya Balimi, Ediss Bebwa baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika fainali ya Mashindano ya Ngoma za Asili ya Bia ya Balimi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment