Tuesday, July 17, 2012

MANJI, SANGA WAPONGEZWA TFF

Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuph Manji (kulia) akiwa na makamu wake Clement Sanga. Picha: Bongostaz.blogspot.com


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeupongeza uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ushindi waliopata wajumbe wapya sita waliochaguliwa kuingia kwenye Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wanachama wa Yanga waliohudhuria uchaguzi huo walivyo na imani kwao.


Wambura alisema TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambayo hivi sasa ina vinara wapya, na kwamba wana changamoto kubwa ya kuhakikisha wanaendesha shughuli za klabu hiyo kwa kuzingatia katiba na kanuni.


Iliongeza taarifa hiyo kwamba TFF pia inatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga chini ya Jaji Mkwawa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na kanuni.


Katika uchaguzi huo ulioanza Jumapili na kumalizika alfajiri ya Jumatatu, Yusuph Manji alishinda uenyekiti kwa asilimia 97 za kura zote, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikienda kwa Clement Sanga.
 Walioshinda nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji walikuwa Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na Geroge Manyama.

Huu hapa ni mtiririko wa matokeo kamili ya kura walizopata wagombea:

Nafasi ya Mwenyekiti:

Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6% na Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:

Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23% na Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi za Ujumbe:

Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249) na Yono Kivela (123)No comments:

Post a Comment