Saturday, July 7, 2012

MAN UNITED YAMUUZA PARK JI-SUNG KWA QPR

Park Ji-Sung akilia wakati alipotangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Korea Kusini Januari 31, 2011 mjini Seoul, Korea Kusini. Park alistaafu baada ya Korea Kusini kushinda 3-2 dhidi ya Uzbekistan katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Asia.
Hata mkija mia.... Park Ji-Sung (katikati) wakati wa mechi dhidi ya Man City.

QUEENS Park Rangers wamekubali dili la kumsajili kiungo Park Ji-sung kutoka Manchester United.

Maafikiano hayo, ambayo yatakuwa na thamani ya paundi milioni 5, yatawashuhudia QPR wakilipa ada ya awali ya paundi milioni 2 kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Korea Kusini amecheza mechi 133 za Ligi Kuu ya England akiwa na Man United tangu alipojiunga nayo akitokea PSV Eindhoven mwaka 2005, na amefunga magoli 19.

Ametwaa makombe manne ya ubingwa wa Ligi Kuu wa England moja la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na United.

Baada ya kuanza soka lake la kulipwa katika klabu ya Japan ya Kyoto Purple Sanga, Park alionyesha kiwango kikubwa timu yake ya taifa ikifuzu kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia 2002, ambapo walikuwa wenyeji wenza.

Kiwango hicho kilimshuhudia akimfuata kocha wake wa taifa Guus Hiddink katika klabu ya PSV Eindhoven, ambako alicheza miaka mitatu kabla ya kukamilisha uhamisho uliogharimu paundi milioni 4 wa kutua Old Trafford, ambako alikuwa akitegemewa katika nafasi za viungo wa kocha Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment