Gomez (katikati) akiwa mwenye huzuni tele baada ya kipigo walichopata kutoka kwa Italia. |
Khedira |
Mtazame Ozil anavyolia kwa uchungu baada ya kutolewa... eti ni kweli yeye na wenzake hawana uzalendo? |
NOTA wa timu ya taifa ya soka ya Ujerumani, ambao bado wanaugulia
machungu ya kipigo cha 2-1 katika mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 dhidi
ya Italia wiki iliyopita, sasa wanashutumiwa vikali kwa kutokuwa wazalendo
kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kutoimba wimbo wa taifa.
Wachezaji wengi wa Ujerumani, wakiwemo Mario Gomez, Mesut
Ozil, Bastian Schweinsteiger, Sami Khedira na Manuel Nuer wanadaiwa kuwa walibaki
kimya wakati wimbo wa taifa lao ukipigwa uwanjani mjini Warsaw Alhamisi
iliyopita, huku wachezaji wote wa Italia
wakionekana kuimba wimbo wao wa taifa kwa furaha.
Nchini Ujerumani, serikali za shirikisho huamua kama
watoto wajifunze wimbo wa taifa wawapo shuleni ama la. Kinyume chake, kwa
wahafidhina wa Bavaria ni lazima kujifunza wimbo huo, wakati mjini Berlin jambo
hilo hutegemeana na uamuzi wa walimu wenyewe.
No comments:
Post a Comment