IKIWA ni sehemu ya udhamini wake
kwa klabu ya Yanga, bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imekabidhi Sh. Milioni
20 kwa klabu hiyo kwa ajili ya mkutano mkuu utakaofanyika sambamba na uchaguzi
wa uongozi mpya Julai 15, mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,
George Kavishe alisema: “Kilimanjaro Premium Lager inatambua wajibu wake na ina
nia ya dhati kuendeleza soka. Kwa kwa kuzingatia hilo tungependa kuona
maendeleo ya Yanga na ndio maana tunaiunga mkono klabu hii katika mkutano wake
mkuu. Tunatambua kuwa hii ni klabu kubwa yenye historia kubwa na hivyo
tunaamini kuwa inahitaji kuwa na uongozi bora, imara na madhubuti.
“Tunatambua wajibu wetu kama
wadhamini wakuu wa Yanga katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea
kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la
Tanzania kwenye kilele cha mafanikio”
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro pia
aliwasihi wajumbe wa mkutano mkuu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo
kwa kufanya uchaguzi wenye amani na kuchagua viongozi watakaofanya kazi kwa
maslahi ya klabu.
No comments:
Post a Comment