Sunday, July 1, 2012

KANOUTE NAYE AFUATA ‘MIHELA’ CHINA

 

Tisha mbaya...! Hapa Kanoute akionyesha vitu vyake wakati akiichezea Sevilla katika mechi mojawapo ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispani.  
Kanoute akionyesha jezi ya klabu yake mpya leo. Imeandikwaje? Mmmhh... sijui STRAIKA! 

SEVILLE, Hispania
MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Mali, Frederic Kanoute ametua nchini China leo kujiunga na klabu ya Beijing Guoan inayoshiriki Chinese Super League, Ligi Kuu ya China.
Awali, mshambuliaji huyo aliyekuwa akiichezea Sevilla inayoshiriki La Liga, Ligi Kuu ya Hispania, alisema mwanozni mwa wiki kuwa anaangalia uwezekano wa kuhamia Mashariki ya Kati, China na Marekani.
Na sasa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Guoan, timu inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya China, ikiachwa kwa pointi saba na vinara Guangzhou Evergrande.
Kanoute alisajiliwa na Sevilla mwaka 2005 baada ya kuichezea Tottenham kwa miaka miwili na kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa klabu hiyo, akifunga mabao 136 katika mechi 290.
Wakati akiwa Hispania, Kanoute alitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka 2007 na pia aliisaidia Sevilla kutwaa makombe mawili ya Uefa, taji moja la Uefa Super Cup, makombe mawili ya Kombe la Mfalme na taji moja la Hispania la Supercopa.
Hivi karibuni, mshambuliaji mwingine nyota wa Afrika, Didier Drogba alisajiliwa na klabu ya China ya Shanghai Shenhua na ataripoti Julai 13 baada ya kumaliza mkataba wake na klabu yake ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment