Monday, July 2, 2012

INIESTA ACHAGULIWA MWANASOKA BORA EURO 2012


Iniesta (kushoto) akiwa na Cesc Fabregas kwenye Uwanja wa Ndege wa Barajas mjini Madrid, leo
 Andres Iniesta (kushoto) akitembea na Sergio Busquets (katikati) na Victor Valdes wakati timu hiyo ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Barajas mjini Madrid, leo.

KIEV, Ukraine
KIUNGO Andres Iniesta, aliyeisaidia Hispania kutwaa taji la pili mfululizo la michuano ya Euro nchini Poland na Ukraine alitangazwa leo kuwa Mwanasoka Bora wa Euro 2012 na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA). 

Iniesta alikuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Hispania kilichoshinda 4-0 dhidi ya Italia katika mechi yao ya fainali ya Euro 2012 juzi wakati mabingwa hao watetezi walipoandika rekodi kwa kuwa nchi ya kwanza kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo. 

Andy Roxburgh, mkuu wa kurugenzi ya ufundi ya UEFA, aliwaambia waandishi wa habari: "Andrea Pirlo aling’ara katika kikosi cha Italia, Xavi alishinda tuzo hii katika michuano iliyopita na angeweza pia kuitwaa tena. Xabi Alonso alionyesha kiwango cha juu lakini Iniesta alipeleka ujumbe kuhusiana na ubunifu na umakini na pia alicheza kwa kiwango bora kabisa katika kila mechi." 

Kikosi cha wachezaji bora wa UEFA katika fainali za Euro 2012:
Makipa; Gianluigi Buffon (Italia), Iker Casillas (Hispania) na Manuel Neuer (Ujerumani) 

Mabeki: Gerard Pique (Hispania), Fabio Coentrao (Ureno), Philipp Lahm (Ujerumani), Pepe (Ureno), Sergio Ramos (Hispania), Jordi Alba (Hispania) 

Viungo: Daniele De Rossi (Italia), Steven Gerrard (England), Xavi (Hispania), Andres Iniesta (Hispania), Sami Khedira (Ujerumani), Sergio Busquets (Hispania), Mesut Ozil (Ujerumani), Andrea Pirlo (Italia), Xabi Alonso (Hispania) 

Mastraika: Mario Balotelli (Italia), Cesc Fabregas (Hispania), Cristiano Ronaldo (Ureno), Zlatan Ibrahimovoic (Sweden), David Silva (Hispania).

No comments:

Post a Comment