Wednesday, July 11, 2012

HUKUMU KESI YA PROF. MAHALU YAPIGWA KALENDA


Prof. Ricky Costa Mahalu (kushoto mbele) akiwa na mwanasheria Alex Mgongolwa katika siku mojawapo ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hukumu iliyotarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusiana na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 inayomkabili balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu (63) imeahirishwa mahakamani hapo hadi tarehe 9 ya mwezi ujao.

Hakimu Katemana ndiye aliyeahirisha kesi hiyo, akitoa sababu kuwa ni kukosekana kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Illivin Mgeta aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo lakini leo akakosekana kwavile anakabiliwa na majukumu mengine.

Awali, katika kesi hiyo, upande wa mashtaka unaoongozwa na mawakili waandamizi wa serikali, Ponsiano Lukosi, Vincent Haule na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin, uliita mashahidi saba na vielelezo tisa vikiwemo mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi jijini Rome, Italia na upande wa utetezi uliita mashahidi watatu, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.

No comments:

Post a Comment