Wednesday, July 18, 2012

HAPPY 'BESDEI' MADIBA... MANDELA ATIMIZA MIAKA 94

Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton akimtembelea Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, katika picha hii iliyopigwa jana (Julai 17, 2012). Mandela anasherehekea kutimiza umri wa miaka 94 leo Julai 18. Picha: REUTERS

RAIS wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela leo anatimiza miaka 94 tangu alipozaliwa.

Siku ya kuzaliwa kwake pia inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake katika kuikomboa Afrika Kusini dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Na nchini Afrika Kusini kwenyewe Nelson Mandela, ataadhimisha siku hii na familia yake na Mmarafiki huku shughuli mbalimbali zikiandaliwa nchini humo kama katika kusherehekea siku hii.

Mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, amesema kuwa Mzee Mandela anaheshimiwa na watu wengi nchini humo, wakitambua juhudi zake za kupigania Uhuru wa Taifa hilo lilolokuwa likiongozwa kirasmi na ubaguzi wa rangi.

Ripoti zinasema raia wa nchi hiyo hii leo watajitolea kufanya kazi ya kuwasaidia wasiojiweza kwa muda wa dakika sitini na saba kama njia moja ya kuadhimisha siku hii.

Mandela aliachiliwa huru kutoka gerezani akiwa na umri wa miaka 67.

Alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini mwaka wa 1994.

No comments:

Post a Comment