Sunday, July 15, 2012

DROGBA ALIVYOTUA CHINA NA KUPOKEWA KIFALME, ASHUHUDIA TIMU YAKE 'KIMEO' IKICHARUKA DHIDI YA MAHASIMU NA KUSHINDA 3-1

Katua na kizizi nini? Straika Didier Drogba akitambulishwa uwanjani na kukabidhiwa jezi atakayovaa na nahodha msaidizi wa klabu yake mpya ya Shanghai Shenhua, Yu Tao. Baada ya utambulisho wake, Shenhua ambayo ilikuwa ikisuasua ilicharuka na kushinda 3-1 jana dhidi ya mahasimu wao Beijing Guo'an na kukwea kutoka nafasi ya pili mkiani hadi katika nafasi ya 12 kati ya timu 16 zinazoshiriki Chinese Super League, ligi kuu ya China.
Shabiki wa Shanghai Shnhua aliyechizikka na ujio wa Didier Drogba akiwa na bango la kuashiria mapokezi yake jana..
Mashabiki waliojitokeza na mabango kumpokea Drogba
Drogba akisalimia mashabiki uwanjani kabla ya utambulisho wake rasmi jana.
Hapa ni baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
Drogba hapa ni kama haamini kutokana na nyomi la mashabiki waliofika uwanja wa ndege kumpokea.
Drogba akilindwa vikali na 'manjagu' wa China baada ya kuwasilia kwenye uwanja wa ndege
Mashabiki wakimzonga Drogba baada ya kwenye uwanja wa ndege jijini Shanghai, jana.
Mashabiki wengine walifika uwanjani na rundo la maua ili kumpokea Drogba. Hata hivyo, polisi hawakuwa mbali na straika huyu ili kumhakikishia ulinzi madhubuti.
SHANGHAI, China
Straika wa timu ya taifa ya Ivory Coast,  Didier Drogba ametua China na kupata mapokezi ya kifalme kabla ya kuanza kutumikia mkataba wake wa miaka miwili na nusu kuichezea klabu ya Shanghai Shenhua.

Mamia ya mashabiki wa klabu yake inayohaha katika Chinese Super League, Ligi Kuu ya China walijitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Pudong jijini Shanghai kumpokea mshambuliaji huyo mwenye miaka 34 na nyota wa zamani wa Chelsea.

Mshahara wa wiki wa Drogba ulioripotiwa kuwa dola za Marekani 300,000 (Sh. Milioni 460) unamfanya awe miongoni mwa wanasoka wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.

Drogba ni miongoni mwa nyota wengi wa kigeni waliotimkia China hivi karibuni.

Katika klabu yake hiyo mpya ya Shanghai Shenhua, anaungana na straika mwenzake wa zamani wa Chelsea, Nicolas Anelka at.

Mara tu baada ya kuwasili, Drogba alisisitiza kwamba hakujiunga na klabu hiyo ili kufuata fedha.

Alisema: "Ingekuwa rahisi kwangu kubaki Ulaya, lakini nimechagua China. Fedha kwangu si kitu muhimu sana. Niko hapa kwa ajili ya kupata changamoto mpya."

"Niliamua kuja hapa kwa sababu rais wa klabu aliponifuata, niliangalia mipango ya baadaye ya timu na kuvutiwa nayo ... nataka kusaidia mchakato wa kukuza mchezo wa soka nchini China," Drogba aliwaambia waandishi wa habari.


"Kwakweli, sikuja hapa kwa nia ya kutengeneza fedha. Nimekuja hapa kwa sababu ya kufuata changamoto mpya kabisa kulinganisha na zile nilizokumbana nazo hapo kabla barani Ulaya.

AKIRI TIMU YAKE KIMEO
"Matokeo ya timu yangu sio amzuri sana. Lakini mnajua, mzunguko wa pili wa msimu wa ligi ndio kwanza umeanza na, nadhani tunao muda wa kujirekebisha na kupata matokeo mazuri na kuiweka timu katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi," Drogba alisema.

"Kwa kushirikiana na wenzangu, tutacheza kadri ya uwezo wetu. Na nimekuja hapa kutwaa ubingwa wa ligi, sikuja hapa kwa ajili ya kuanza safari yangu ya kustaafu soka au sababu nyingine ya namna hiyo.

"Nataka watu wathibitishe na kuelewa kwamba nimekuja hapa kushinda. Sikuja hapa kukaa na kupumzika tu."

Baada ya utambulisho wake jana, Drogba sasa anaweza kuichezea timu Shanghai katika mechi yake ya kwanza wiki ijayo wakati watakapocheza ugenini dhidi ya Changchun.

Straika huyo alifunga mabao 157 katika mechi 341 alizoichezea Chelsea na hivi karibuni aliisaidia timu yake ya zamani kutwaa kwa mara ya kwanza taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuifungia bao muhimu la kusawazisha katika dakika 90 za kawaida na mwishowe akafunga penati iliyowapa ubingwa wakati wa hatua ya ‘matuta’.

No comments:

Post a Comment