Monday, July 9, 2012

DIAMOND, SHETTA, JOH MAKINI, FID Q WALIVYOPAGAWISHA TAMASHA LA WAJANJA WA VODACOM MTWARA

Cheki mauno sasa... Nyota wa Bongofleva, Diamond Platnumz, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la WAJANJA kwenye Uwanja wa  Nang’wanda mkoani Mtwara jana. Tamasha hilo limefanyika katika mikoa mitatu nchini na litamalizikia mkoa wa Tanga Jumapili hii likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni wa Vodacom kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa Sh. 25 kwenda mtandao wowote na kutumia Facebook na Twitter bure.

Ney wa Mitego akipagawisha wakati wa tamasha hilo...

Mashabiki kibao walikuwepo...

Twende sasa.... chezea Kiduku wewe? Watoto wa Mtwara wakionyesha maujuzi yao wakati wa Tamasha la WAJANJA la Vodacom jana.

Ngosha the Swagga Don.... mkali wa hip hop nchini Fid Q naye alisomeka pande hizo...

Nyeusiiiiiii...... nyeusi hasa! Mkali wa hip hop kutoka pande za Arusha, Joh Makini akiwakilisha.

Hapa ni Da' Stamina President, Shetta (kulia) akiomba watu wa Mtwara "wamdanganye-danganye...."

Nimpende naniiiiii? Wema?

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano, Joseline Kamuhanda (katikati) akipozi kwa picha na wadau katika tamasha la ”Wajanja wa Vodacom” lililofanyika jana katika uwanja wa Nang’wanda mkoani Mtwara. Tamasha hilo limefanyika katika mikoa mitatu hapa nchini na litamalizikia mkoa wa Tanga Jumapili ijayo likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni wa Vodacom kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa Sh.25 kwenda mtandao wowote na kutumia Facebook na Twitter bure.

No comments:

Post a Comment