Tuesday, July 10, 2012

DIAMOND BALOZI MPYA VUTA MKWANJA NA COCA COLA

Wema akikuona wewe....! Balozi wa kampeni mpya ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi mwandamizi wa gazeti la NIPASHE, Somoe Ng’itu, fedha taslim Tsh 50,000 alizojishindia kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika kiwanda cha Coca-Cola Kwanza Mikocheni, Dar es Salaam leo (Julai 10, 2012).

Balozi wa kampeni mpya ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi mfanyakazi wa kampuni ya Sonda Communications, Elizabeth Mmasi, fedha taslim Tsh 100,000 alizojishindia kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika kiwanda cha Coca-Cola Kwanza Mikocheni, Dar es Salaam leo (Julai 10, 2012).

Msanii maarufu nchini Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola uliofanyika katika kiwanda cha Coca-Cola Kwanza Mikocheni, Dar es Salaam leo (Julai 10, 2012). Wengine ni Evans Mlelwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya umma wa Coca-Cola Kwanza (katikati) na Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Feisal Baghazal. Diamond ni balozi wa kampeni hiyo. 

Wateja wa Coca-Cola kujishindia fedha taslim hadi Sh. milioni 1

 
Dar es Salaam Jumanne, Julai 10, 2012 …. Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza leo imezindua promosheni ambayo itawawezesha watumiaji wa vinywaji vyake kujishindia zawadi za fedha taslim hadi Sh. milioni 1. Zawadi nyingine za fedha taslim ni 500,000, 100,000, 50,000, 10,000, 5,000, 2,000, fulana na soda za bure.

Promosheni hii pia ni sehemu ya kampeni kabambe ya Coca-Cola iliyozinduliwa mwezi Aprili ijulikanayo kama sababu bilioni moja za kuthamini Afrika inayowahamasisha wananchi hasa vijana kuwa wazalendo na kujivunia raslimali mbali mbali ambazo nchi za bara la Afrika zimejaliwa kuwa nazo.
   
Promosheni iliyozinduliwa leo itadumu kwa muda wa wiki sita na inafahamika kama Vuta Mkwanja na Coca-Cola. Hii ni fursa nyingine ambayo inatoa nafasi kwa kampuni ya Coca-Cola kuwa karibu zaidi na wateja wake walioko nchi nzima, mijini na vijijini.

“Ni dhahiri kwamba promosheni tunayoizindua hivi leo itasaidia kuboresha maisha ya Watanzania watakaobahatika kushinda zawadi za fedha taslim hasa wale ambao watajishindia ile zawadi kubwa ya Sh. milioni 1”, anasema Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa Coca-Cola Kwanza Evans Mlelwa.

Alisema kwa miaka mingi, Coca-Cola imekuwa ikiendesha promosheni za aina hii ambazo zinawawezesha wateja kujishindia zawadi za fedha taslim na hivyo kusaidia kuwakwamua kiuchumi na promosheni hii ya “Vuta Mkwanja na Coca-Cola ina lengo hilo la kuwawezesha wateja wa Coca-Cola kiuchumi”.

Ili kushiriki, wateja wanatakiwa kukunua vinywaji vya jamii ya Coca-Cola vyenye ujazo wa 350ml na kuangalia chini ya kizibo ili kuona aina ya zawaidi waliojishindia.

Wakati washindi wa fedha taslim kuanzia Tsh 2,000 hadi 10,000 watapewa zawadi zao pale pale kwa wauzaji, washindi wa kuanzia Tsh 50,000 hadi 1m watakabidhiwa zawadi zao kwenye kiwanda cha kilicho karibu. Viwanda hivyo ni Kwanza, Bonite na Nyanza.

Mlelwa ametoa rai kwa wateja wa Coca-Cola na umma wa Watanzania kwa ujumla kushiriki katika promosheni hii ili kujiweka katika nafasi ya kuwa milionea mara moja kwa hisani ya Coca-Cola.
 
Amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Coca-Cola kuendelea kuzalisha na kusambaza vinywaji vyenye ubora wa kimataifa. Vinywaji hivyo ni pamoja na Coca-Cola, Fanta na Sprite.


No comments:

Post a Comment