Wednesday, July 4, 2012

CHUJI AMUOKOA MTUHUMIWA WA WIZI WA MIPIRA YANGA



Dereva wa Yanga, Ramadhani Cops, 'akimburuza' kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Dereva wa Yanga, Ramadhani Cops, 'akimburuza' kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Dereva wa Yanga, Ramadhani Cops, 'akimburuza' kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Athumani Idd 'Chuji' wa Yanga akiingilia kumuokoa kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Athumani Idd 'Chuji' wa Yanga akiingilia kumuokoa kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Athumani Idd 'Chuji' wa Yanga akimuondoa kijana kutoka kwa watu waliokuwa wakimshambulia kijana aliyeshukiwa kuiba mpira wa timu hiyo leo.

Na Sanula Athanas
KIUNGO wa klabu ya Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’, leo asubuhi aliokoa kuokoa maisha ya kijana aliyetuhumiwa kuiba mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


Tukio hilo lililosababisha mazoezi kusimama kwa takriban dakika sita, lilishuhudia mashabiki wa soka waliofika uwanjani hapo wakimpa kipigo kijana huyo bila huruma.


Kijana huyo aliletwa uwanjani hapo "akiburutwa" na dereva wa Yanga, Ramadhani Cops, ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakilinda vifaa vya Yanga wakati wa mazoezi hayo.

Kijana huyo aliyekuwa amevalia fulana nyekundu ya klabu ya Manchester United ya Uingereza, alijikuta akiongezwa mkong'oto na mashabiki wengine waliokuwa wakidai "ametumwa na Simba".


Kiungo wa zamani wa Simba, Chuji ambaye alikuwa uwanjani, alimuonea huruma kijana huyo na akakimbia haraka na kuingia katikati ya mashabiki waliokuwa wakitoa kipigo na kuwaasa wamsamehe.


“Imetosha, imetosha jamani, naomba tumsamehe jamani, mwachie kijana wa watu, naamini amejifunza kwa kipigo hiki, naomba tumsamehe,” alisema Chuji.


Chuji alimsindikiza kijana huyo hadi nje ya uwanja na kumtaka aache tabia hiyo akimwambia, “watakuchoma moto, unatakufa kwa kuiba mipira ya klabu.”


Dereva wa Yanga aliiambia STRAIKA kuwa kijana huyo alikamatwa na baada ya kukimbia na mpira uliopigwa shuti na kutoka nje ya uzio.

"Tuko watu watatu hapa tunaangalia usalama wa vifaa vya timu yetu. Baada ya mpira kutoka, yule kijana aliuchukua na kuanza kukimbia… nikaanza kumfukuza lakini nilipomkaribia akatoa kisu na kuanza kunitishia. Nilipanga nimpeleke kituo cha polisi lakini kwa kuwa wachezaji wamekataa sina budi kumsamehe,” alisema dereva huyo.


Mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga wanautumia uwanja wa bora kwa ajili ya kujiandaa na kampeni mpya za kutetea taji lao katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 jijini Dar es Salaam.

--------

No comments:

Post a Comment